Yeremia 44
1 Neno hili lilimjia Yeremia kuhusu Wayahudi wote walioishi Misri, huko Migdoli, Tapanesi na Memfisi, katika nchi ya Pathrosi, kusema:
2 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Mliona maangamizi makubwa niliyoyaleta juu ya Yerusalemu na juu ya miji yote ya Yuda. Leo imeachwa ukiwa na magofu
3 kwa sababu ya uovu waliokuwa wameufanya. Walinikasirisha kwa kufukiza uvumba na kwa kuabudu miungu mingine ambayo haikuwahi kujulikana kwao, wala kwenu na mababu zenu.
4 Tena na tena, niliwatuma watumishi wangu manabii ambao walisema, ‘Msifanye jambo hili la kuchukiza ambalo nalichukia!’
5 Lakini hawakusikiliza wala hawakujali, hawakugeuka ili kuuacha uovu wao, wala hawakuacha kufukiza uvumba kwa miungu mingine.
6 Kwa hiyo hasira yangu kali ilimwagika, ikawaka dhidi ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, na kuifanya ukiwa na magofu kama ilivyo leo.
7 “Basi hili ndilo Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Kwa nini kujiletea maafa makubwa kama haya juu yenu kwa kujikatilia mbali kutoka Yuda wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, hata kujiacha bila mabaki?
8 Kwa nini kuichochea hasira yangu kwa kazi ya mikono yenu, kuifukizia uvumba miungu mingine huko Misri, mahali mlipokuja kuishi? Mtajiangamiza wenyewe na kujifanya kitu cha kulaania na shutumu miongoni mwa mataifa yote duniani.
9 Je, mmesahau uovu uliotendwa na baba zenu, na wafalme na malkia wa Yuda, na uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na barabara za Yerusalemu?
10 Hadi leo hawajajinyenyekeza au kuonesha heshima, wala hawajafuata sheria yangu na amri nilizoweka mbele yenu na baba zenu.
11 “Kwa hiyo, hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Mimi nimekusudia kuleta maafa juu yenu, na kuiangamiza Yuda yote.
12 Nitawaondoa mabaki ya Yuda waliokusudia kwenda Misri kukaa huko. Wote wataangamia huko Misri, wataanguka kwa upanga au kufa kwa njaa. Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana, watakufa kwa upanga au njaa. Watakuwa kitu cha kulaania na cha kutisha, cha laumu na shutumu.
13 Nitawaadhibu wanaoishi Misri kwa upanga, njaa na tauni kama nilivyoiadhibu Yerusalemu.
14 Hakuna hata mmoja wa mabaki ya Yuda ambaye ameenda kuishi Misri atakayeepuka au kunusurika ili kurudi katika nchi ya Yuda, ambayo wanaitamani sana kurudi na kuishi ndani yake, hakuna hata mmoja atakayerudi isipokuwa wakimbizi wachache.”
15 Kisha wanaume wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakifukiza uvumba kwa miungu mingine, pamoja na wanawake wote waliokuwako, yaani kusanyiko kubwa na watu wote walioishi nchi ya Misri na Pathrosi, wakamwambia Yeremia,
16 “Hatutausikiliza ujumbe uliotuambia katika jina la Mwenyezi Mungu!
17 Hakika tutafanya kila kitu tulichosema tutakifanya: Tutafukiza uvumba kwa Malkia wa Mbinguni na tutammiminia sadaka zetu za kinywaji kama sisi na baba zetu, wafalme na wakuu wetu tulivyofanya katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu. Wakati ule tulikuwa na chakula tele, tulikuwa matajiri wala hatukupata dhara lolote.
18 Lakini tangu tulipoacha kumfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka za kinywaji, hatupati chochote, na tumekuwa tukiangamizwa kwa upanga na njaa.”
19 Wanawake wakaongeza kusema, “Tulipomfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni, na kummiminia sadaka zetu za kinywaji, je, waume zetu hawakujua kwamba tulikuwa tukitengeneza maandazi kwa mfano wake, na kummiminia yeye sadaka za kinywaji?”
20 Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake waliokuwa wakimjibu,
21 “Je, Mwenyezi Mungu hakukumbuka na kufikiri kuhusu uvumba uliofukizwa katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu na ninyi pamoja na baba zenu, wafalme wenu, maafisa wenu na watu wa nchi?
22 Mwenyezi Mungu alipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaaniwa na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo.
23 Kwa sababu mmefukiza uvumba na kufanya dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, nanyi hamkumtii wala kufuata sheria yake au amri zake au maagizo yake, maafa haya yamekuja juu yenu, kama mnavyoona sasa.”
24 Kisha Yeremia akawaambia watu wote, pamoja na wanawake, “Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi watu wote wa Yuda mlioko Misri.
25 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Ninyi na wake zenu mmeonesha kwa matendo yenu kile mlichoahidi mliposema, ‘Hakika tutatimiza nadhiri tulizoziweka za kumfukizia uvumba na kummiminia sadaka za kinywaji Malkia wa Mbinguni.’ “Endeleeni basi, fanyeni yale mliyoahidi! Timizeni nadhiri zenu!
26 Lakini sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi Wayahudi wote mnaoishi Misri: ‘Ninaapa kwa Jina langu lililo kuu,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘kwamba hakuna hata mmoja atokaye Yuda anayeishi popote Misri ambaye kamwe ataomba tena kwa Jina langu au kuapa, akisema, “Hakika kama Bwana Mungu Mwenyezi aishivyo.”
27 Kwa maana ninawaangalia kwa ajili ya madhara, wala sio kwa mema. Kila Myahudi aliyeko nchi ya Misri ataangamia kwa upanga au kwa njaa, hadi wote waangamie.
28 Wale watakaonusurika upanga na kurudi katika nchi ya Yuda kutoka Misri watakuwa wachache sana. Ndipo mabaki wote wa Yuda waliokuja kuishi Misri watajua ni neno la nani litakalosimama: kwamba ni langu au ni lao.
29 “ ‘Hii itakuwa ndiyo ishara kwenu kwamba nitawaadhibu mahali hapa, asema Mwenyezi Mungu, ili mpate kujua kuwa onyo langu la madhara dhidi yenu hakika litatimizwa.’
30 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Nitamtia Farao Hofra mfalme wa Misri mikononi mwa adui zake wanaoutafuta uhai wake, kama nilivyomtia Sedekia mfalme wa Yuda mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, adui aliyekuwa akiutafuta uhai wake.’ ”
Marejeleo mtambuka
223
- 1Jer 46:14, Isa 11:11, Exo 14:2, Isa 19:13, Ezk 30:14, Ezk 30:16, Ezk 29:14, Jer 2:16
- 2Jer 34:22, Jer 9:11, Isa 6:11, Mic 3:12, Jer 4:7, Jer 39:1–8, Lev 26:43, Deu 29:2
- 3Deu 29:26, Deu 13:6, Deu 32:17, Dan 9:5, Neh 9:33, Jer 44:8, Ezk 8:17–18, Jer 2:17–19
- 4Jer 26:5, Jer 7:13, Jer 7:25, Jer 16:18, Jer 29:19, Zec 7:7, 2Ch 36:15, Ezk 8:10
- 5Jer 19:13, Jer 11:10, Zec 7:11–12, Isa 48:18, Isa 48:4, 2Ch 36:16, Jer 11:8, Jer 44:17–21
- 6Jer 7:20, Isa 51:20, Jer 7:34, Jer 42:18, Ezk 8:18, Jer 21:5, Isa 51:17, Isa 6:11
- 7Hab 2:10, Jer 51:22, Ezk 33:11, Num 16:38, Jos 6:21, Pro 15:32, 1Sa 15:3, Jer 7:19
- 8Jer 42:18, Jer 25:6–7, Jer 44:3, 2Ch 7:20, 2Ki 17:15–17, 1Co 10:21–22, Jer 18:16, 1Ki 9:7–8
- 9Jer 7:17–18, Dan 9:5–8, Jos 22:17–20, Jer 44:21, Jer 44:15–19, Ezr 9:7–15
- 10Pro 28:14, Jer 8:12, 1Pe 5:6, Rev 15:4, Ezk 9:4, Isa 57:15, Luk 23:40, 2Ch 12:6–12
- 11Jer 21:10, Lev 20:5–6, Psa 34:16, Amo 9:4, Lev 17:10, Lev 26:17, Ezk 14:7–8, Ezk 15:7
- 12Jer 42:15–18, Jer 42:22, Isa 65:15, Isa 1:28, Jer 44:7–8, Jer 29:18, Jer 29:22, Hos 4:6
- 13Jer 44:27–28, Jer 11:22, Jer 43:11, Jer 24:10, Jer 42:18, Jer 21:9
- 14Rom 9:27, Jer 22:26–27, Jer 44:27–28, Isa 10:20, Jer 42:17, Isa 4:2, Heb 2:3, Rom 2:3
- 15Jer 5:1–5, Pro 11:21, Neh 13:26, Mat 7:13, Gen 19:4, 2Pe 2:1–2, Isa 1:5
- 16Luk 19:27, Job 21:14–15, Dan 3:15, Isa 3:9, Exo 5:2, Jer 16:15–17, Jer 18:18, Jer 8:12
- 17Jer 7:18, Neh 9:34, Deu 23:23, Jer 44:21, Php 3:19, Exo 16:3, Jer 44:25, Ezk 20:8
- 18Mal 3:13–15, Num 11:5–6, Job 21:14–15, Jer 40:12, Psa 73:9–15
- 19Jer 7:18, Jer 44:15, Gen 3:16–17, 2Ch 21:6, Gen 3:6, Gen 3:11–12, Num 30:6–7, Deu 7:3–4
- 21Jer 44:17, Psa 79:8, Isa 64:9, Jer 44:9, Jer 11:13, Jer 14:10, Hos 7:2, Amo 8:7
- 22Jer 25:18, Jer 25:11, Jer 18:16, Isa 7:13, Isa 43:24, Jer 25:38, Mal 2:17, Jer 44:12
- 23Dan 9:11–12, 1Ki 9:9, Neh 13:18, Psa 119:150, Lam 1:8, 2Ch 36:16, Jer 7:13–15, Psa 119:155
- 24Jer 43:7, Jer 44:26, Jer 44:15–16, Jer 42:15, Mat 11:15, 1Ki 22:19, Ezk 2:7, Ezk 20:32–33
- 25Mat 14:9, Isa 28:15, Jas 1:14–15, Jer 44:15–19, Act 23:12–15, Job 34:22, Ezk 20:39, Jud 1:13
- 26Ezk 20:39, Gen 22:16, Heb 6:13, Psa 50:16, Amo 6:8, Jer 4:2, Jer 5:2, Isa 48:1–2
- 27Jer 31:28, 2Ki 21:14, Jer 1:10, Jer 44:18, Ezk 7:6, Jer 21:10, Jer 44:12
- 28Jer 44:14, Isa 10:19, Isa 27:12–13, Jer 44:25–26, Isa 46:10–11, Psa 33:11, Isa 28:16–18, Jer 44:29
- 29Pro 19:21, Mat 24:15–16, Isa 40:8, Jer 44:30, 1Sa 2:34, Luk 21:20–21, Luk 21:29–33, Mat 24:32–34
- 302Ki 25:4–7, Jer 43:9–13, Jer 34:21, Ezk 30:21, Jer 39:5–7, Ezk 29:1–21, Jer 52:8–11, Ezk 31:18–32:32