2 Mambo Ya Nyakati 12
1 Baada ya ufalme wa Rehoboamu kuimarika naye akawa na nguvu, yeye na Waisraeli wote waliiacha Torati ya Mwenyezi Mungu.
2 Kwa sababu hawakuwa waaminifu kwa Mwenyezi Mungu, Shishaki mfalme wa Misri akashambulia Yerusalemu katika mwaka wa tano wa utawala wa Mfalme Rehoboamu.
3 Akiwa na magari ya vita elfu moja mia mbili, wapanda farasi elfu sitini, na idadi isiyohesabika ya majeshi ya Walibia, Wasukii na Wakushi waliokuja pamoja naye kutoka Misri.
4 Akateka miji ya Yuda yenye ngome, akaendelea hadi Yerusalemu.
5 Ndipo nabii Shemaya akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda waliokuwa wamekusanyika huko Yerusalemu kwa ajili ya hofu ya Shishaki naye akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, ‘Ninyi mmeniacha, kwa hiyo, mimi nami sasa ninawaacha mkononi mwa Shishaki.’ ”
6 Viongozi wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, “Mwenyezi Mungu ni mwenye haki.”
7 Mwenyezi Mungu alipoona kwamba wamejinyenyekeza, neno hili la Mwenyezi Mungu likamjia Shemaya: “Maadamu wamejinyenyekeza, sitawaangamiza, bali hivi karibuni nitawapatia wokovu. Ghadhabu yangu haitamwagwa juu ya Yerusalemu kupitia kwa Shishaki.
8 Hata hivyo, watamtumikia Shishaki ili wapate kujifunza tofauti kati ya kunitumikia mimi na kuwatumikia wafalme wa nchi nyingine.”
9 Shishaki mfalme wa Misri alipoishambulia Yerusalemu, alichukua hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa amezitengeneza.
10 Kwa hiyo Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba badala ya zile za dhahabu na kuzikabidhi kwa majemadari wa ulinzi wa zamu kwenye ingilio la jumba la mfalme.
11 Kila wakati mfalme alipoenda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu walinzi walienda pamoja naye wakiwa wamebeba hizo ngao na baadaye walizirudisha kwenye chumba cha ulinzi.
12 Kwa sababu Rehoboamu alijinyenyekeza, hasira ya Mwenyezi Mungu ikageukia mbali naye, hakuangamizwa kabisa. Kukawa na hali nzuri katika Yuda.
13 Mfalme Rehoboamu akajiweka imara katika Yerusalemu na akaendelea kuwa mfalme. Alikuwa na umri wa miaka arobaini na moja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na saba, mji ambao Mwenyezi Mungu alikuwa ameuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli ili aliweke Jina lake humo. Mama yake aliitwa Naama, na alikuwa Mwamoni.
14 Rehoboamu akatenda maovu kwa sababu hakuuelekeza moyo wake katika kumtafuta Mwenyezi Mungu.
15 Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwa na vita vya mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu.
16 Rehoboamu akalala na baba zake, akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Abiya mwanawe akawa mfalme baada yake.
Marejeleo mtambuka
107
- 12Ch 11:17, 2Ch 12:13, 2Ch 26:13–16, 1Ki 14:22–24, Hos 13:1, 1Ki 12:17, Hos 13:6–8, 1Ki 9:9
- 21Ki 11:40, 2Ch 7:19–20, Jer 44:22–23, Isa 63:10, Lam 5:15, Psa 106:43–44, Jer 2:19, 1Ki 14:24–26
- 32Ch 16:8, Nam 3:9, Dan 11:43, Gen 10:6–8, Jdg 6:5, 2Ch 14:12, 2Ch 14:9, 2Sa 10:18
- 42Ch 11:5–12, Isa 36:1, Jer 5:10, Isa 10:11, Isa 8:8, 2Ki 18:17
- 52Ch 15:2, 2Ch 11:2, 1Ki 12:22, 2Ch 12:1–2, Jer 2:19, Jer 5:19, Jdg 10:9–14, 2Sa 24:14
- 6Exo 9:27, Dan 9:14, Jdg 1:7, Hos 5:15, Psa 129:4, Exo 10:3, 2Ch 33:23, 2Ch 32:26
- 72Ch 34:25, Isa 42:25, 1Ki 21:28–29, Jer 3:13, Amo 7:6–8, Luk 15:18–21, Rev 14:10, 2Ki 13:4–7
- 8Deu 28:47–48, Isa 26:13, Jer 10:24, Jdg 3:1, Hos 8:10, Neh 9:36
- 91Ki 10:16–17, 2Ch 9:15–16, 2Ki 16:8, 1Ki 14:25–28, Lam 1:10, 1Ki 15:18, 2Ki 18:15–16
- 101Ki 14:27, 2Sa 23:23, 2Sa 8:18, 1Ch 11:25, Lam 4:1, Sng 3:7–8
- 122Ch 19:3, Lam 3:22, 2Ch 12:6–7, 1Ki 14:13, 2Ch 33:12–13, Gen 18:24, Lam 3:42, Isa 57:15
- 131Ki 14:21, 2Ch 6:6, Deu 12:5, Deu 23:3, Deu 12:11, Ezk 48:35, Exo 20:24, 2Ch 13:7
- 142Ch 19:3, 1Co 15:58, Isa 45:19, 1Co 16:13, Isa 55:6–7, Ezk 33:31, 2Ch 30:19, Psa 105:3–4
- 152Ch 9:29, 2Ch 12:5, 2Ch 13:22, 1Ki 12:22, 1Ki 14:29–30
- 162Ch 11:20, 1Ki 14:29–31, Mat 1:7, 2Ch 13:1, 1Ch 3:10