Zaburi 119
1 Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika Torati ya Mwenyezi Mungu.
2 Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote.
3 Wasiofanya lolote lililo baya, wanaoenenda katika njia zake.
4 Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu.
5 Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako!
6 Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote.
7 Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki.
8 Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa.
9 Kijana aisafishe njia yake jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
10 Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.
11 Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.
12 Uhimidiwe, Ee Mwenyezi Mungu; nifundishe maagizo yako.
13 Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako.
14 Ninafurahia kufuata sheria zako kama mtu afurahiaye mali nyingi.
15 Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako.
16 Ninafurahia maagizo yako, wala sitalipuuza neno lako.
17 Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi; nitalitii neno lako.
18 Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.
19 Mimi ni mgeni duniani, usinifiche amri zako.
20 Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa kwa sheria zako wakati wote.
21 Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa, wanaoenda mbali na amri zako.
22 Niondolee dharau na dhihaka, kwa kuwa ninazishika sheria zako.
23 Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia, mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako.
24 Sheria zako ni furaha yangu, nazo ni washauri wangu.
25 Nimelazwa chini mavumbini, yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.
26 Nilikueleza njia zangu ukanijibu, nifundishe sheria zako.
27 Nijulishe mafundisho ya mausia yako, nami nitatafakari maajabu yako.
28 Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, uniimarishe sawasawa na neno lako.
29 Niepushe na njia za udanganyifu, kwa neema unifundishe sheria zako.
30 Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako.
31 Nimeng’ang’ania sheria zako, Ee Mwenyezi Mungu, usiniache niaibishwe.
32 Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.
33 Ee Mwenyezi Mungu, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika hadi mwisho.
34 Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako na kuitii kwa moyo wangu wote.
35 Niongoze kwenye njia ya amri zako, kwa kuwa huko napata furaha.
36 Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, na siyo kwenye mambo ya ubinafsi.
37 Geuza macho yangu kutoka mambo yasiyofaa, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.
38 Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, ili upate kuogopwa.
39 Niondolee aibu ninayoiogopa, kwa kuwa sheria zako ni njema.
40 Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako.
41 Ee Mwenyezi Mungu, upendo wako usiokoma unijie, wokovu wako sawasawa na ahadi yako,
42 ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, kwa kuwa ninalitumainia neno lako.
43 Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako.
44 Nitaitii amri yako daima, naam, milele na milele.
45 Nitatembea huru, kwa kuwa nimejifunza mausia yako.
46 Nitasema sheria zako mbele za wafalme wala sitaaibishwa,
47 kwa kuwa ninazifurahia amri zako kwa sababu ninazipenda.
48 Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu, nami ninatafakari juu ya maagizo yako.
49 Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, kwa sababu umenipa tumaini.
50 Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.
51 Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka, hata hivyo sitaiacha sheria yako.
52 Ee Mwenyezi Mungu, ninazikumbuka sheria zako za zamani, nazo zinanifariji.
53 Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, ambao wameacha sheria yako.
54 Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu popote ninapoishi.
55 Ee Mwenyezi Mungu, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, nami nitatii sheria yako.
56 Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako.
57 Ee Mwenyezi Mungu, wewe ni fungu langu, nimeahidi kuyatii maneno yako.
58 Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, nihurumie sawasawa na ahadi yako.
59 Nimezifikiri njia zangu na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako.
60 Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako.
61 Hata waovu wanifunge kwa kamba, sitasahau sheria yako.
62 Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki.
63 Mimi ni rafiki kwa wale wote wanaokucha, kwa wote wanaofuata mausia yako.
64 Ee Mwenyezi Mungu, dunia imejaa upendo wako, nifundishe maagizo yako.
65 Mtendee wema mtumishi wako Ee Mwenyezi Mungu, sawasawa na neno lako.
66 Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, kwa kuwa ninaamini amri zako.
67 Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako.
68 Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, nifundishe maagizo yako.
69 Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo, nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote.
70 Mioyo yao ni katili na migumu, bali mimi napendezwa na sheria yako.
71 Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako.
72 Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.
73 Mikono yako iliniumba na kunitengeneza, nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.
74 Wale wanaokucha na wafurahie wanaponiona, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.
75 Ee Mwenyezi Mungu, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu.
76 Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.
77 Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, kwa kuwa naifurahia sheria yako.
78 Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako.
79 Wale wanaokucha na wanigeukie mimi, hao ambao wanazielewa sheria zako.
80 Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, ili nisiaibishwe.
81 Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.
82 Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifariji lini?”
83 Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, bado sijasahau maagizo yako.
84 Mtumishi wako itampasa angoje hadi lini? Ni lini utawaadhibu washtaki wangu?
85 Wenye majivuno wananichimbia mashimo, kinyume na sheria yako.
86 Amri zako zote ni za kuaminika; unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu.
87 Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, lakini sijaacha mausia yako.
88 Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, nami nitatii sheria za kinywa chako.
89 Ee Mwenyezi Mungu, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni.
90 Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, umeiumba dunia, nayo inadumu.
91 Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.
92 Kama nisingefurahia sheria yako, ningeangamia katika taabu zangu.
93 Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.
94 Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako.
95 Waovu wanangojea kuniangamiza, bali mimi ninatafakari sheria zako.
96 Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, lakini amri zako hazina mwisho.
97 Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa.
98 Amri zako zimenipa hekima kuliko adui zangu, kwa kuwa nimezishika daima.
99 Nina akili kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari kuhusu sheria zako.
100 Nina ufahamu kuliko wazee, kwa kuwa ninayatii mausia yako.
101 Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako.
102 Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe.
103 Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu!
104 Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.
105 Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.
106 Nimeapa na nimethibitisha, kwamba nitafuata sheria zako za haki.
107 Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Mwenyezi Mungu, sawasawa na neno lako.
108 Ee Mwenyezi Mungu, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako.
109 Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, sitasahau sheria yako.
110 Waovu wamenitegea mtego, lakini sijayakiuka maagizo yako.
111 Sheria zako ni urithi wangu milele, naam ni furaha ya moyo wangu.
112 Nimekusudia moyoni mwangu kuyafuata maagizo yako hadi mwisho.
113 Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako.
114 Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu, nimeweka tumaini langu katika neno lako.
115 Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu, ili niweze kushika amri za Mungu wangu!
116 Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa.
117 Nitegemeze, nami nitaokolewa, nami daima nitayaheshimu maagizo yako.
118 Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako, kwa maana udanganyifu wao ni bure.
119 Waovu wa nchi unawatupa kama takataka, kwa hivyo nazipenda sheria zako.
120 Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, ninaziogopa sheria zako.
121 Nimetenda yaliyo haki na sawa, usiniache mikononi mwa watesi wangu.
122 Mhakikishie mtumishi wako usalama, usiache wenye kiburi wanidhulumu.
123 Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli.
124 Mtendee mtumishi wako kulingana na upendo wako na unifundishe maagizo yako.
125 Mimi ni mtumishi wako; nipe busara ili niweze kuelewa sheria zako.
126 Ee Mwenyezi Mungu, wakati wako wa kutenda umewadia, kwa kuwa sheria yako inavunjwa.
127 Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu, naam, zaidi ya dhahabu safi,
128 na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili, nachukia kila njia potovu.
129 Sheria zako ni za ajabu, hivyo ninazitii.
130 Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, kunampa mjinga ufahamu.
131 Nimefungua kinywa changu na kuhema, nikitamani amri zako.
132 Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote wale wanaolipenda jina lako.
133 Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako, usiache dhambi yoyote initawale.
134 Niokoe na uonevu wa wanadamu, ili niweze kutii mausia yako.
135 Mwangazie mtumishi wako uso wako na unifundishe amri zako.
136 Chemchemi za machozi zinatiririka machoni yangu, kwa kuwa sheria yako haifuatwi.
137 Ee Mwenyezi Mungu, wewe ni mwenye haki, sheria zako ni sahihi.
138 Sheria ulizoziweka ni za haki, ni za kuaminika kikamilifu.
139 Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu wanayapuuza maneno yako.
140 Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu, mtumishi wako anazipenda.
141 Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa, sisahau mausia yako.
142 Haki yako ni ya milele, na sheria yako ni kweli.
143 Shida na dhiki zimenipata, lakini amri zako ni furaha yangu.
144 Sheria zako ni sahihi milele, hunipa ufahamu ili nipate kuishi.
145 Ee Mwenyezi Mungu, ninakuita kwa moyo wangu wote, nami nitayatii maagizo yako.
146 Ninakuita; niokoe nami nitazishika sheria zako.
147 Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; nimeweka tumaini langu katika neno lako.
148 Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.
149 Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako, Ee Mwenyezi Mungu, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako.
150 Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami, lakini wako mbali na sheria yako.
151 Ee Mwenyezi Mungu, hata hivyo wewe u karibu, na amri zako zote ni za kweli.
152 Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako kwamba umezithibitisha ili zidumu milele.
153 Yaangalie mateso yangu, uniokoe, kwa kuwa sijasahau sheria yako.
154 Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako.
155 Wokovu uko mbali na waovu, kwa kuwa hawatafuti maagizo yako.
156 Ee Mwenyezi Mungu, huruma zako ni kuu, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako.
157 Adui wanaonitesa ni wengi, lakini mimi sitaziacha sheria zako.
158 Ninawatazama wasioamini kwa chuki, kwa kuwa hawalitii neno lako.
159 Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako; Ee Mwenyezi Mungu, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako.
160 Maneno yako yote ni kweli, sheria zako zote za haki ni za milele.
161 Watawala wamenitesa bila sababu, lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako.
162 Nafurahia ahadi zako kama mtu aliyepata mateka mengi.
163 Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo, lakini napenda sheria yako.
164 Ninakusifu mara saba kwa siku, kwa ajili ya sheria zako za haki.
165 Wanaopenda sheria yako wana amani tele, wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza.
166 Ee Mwenyezi Mungu, ninangojea wokovu wako, nami ninafuata amri zako,
167 Ninazitii sheria zako, kwa sababu ninazipenda mno.
168 Nimetii mausia yako na sheria zako, kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako.
169 Ee Mwenyezi Mungu, kilio changu na kifike mbele zako, nipe ufahamu sawasawa na neno lako.
170 Maombi yangu na yafike mbele zako, niokoe sawasawa na ahadi yako.
171 Midomo yangu na ibubujike sifa, kwa kuwa unanifundisha maagizo yako.
172 Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, kwa kuwa amri zako zote ni za haki.
173 Mkono wako uwe tayari kunisaidia, kwa kuwa nimechagua mausia yako.
174 Ee Mwenyezi Mungu, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu.
175 Nijalie kuishi ili nipate kukusifu, na sheria zako zinitegemeze.
176 Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea. Mtafute mtumishi wako, kwa kuwa sijasahau amri zako.
Marejeleo mtambuka
1322
- 1Luk 11:28, Ezk 11:20, Jas 1:25, Psa 128:1, Jhn 13:17, Luk 1:6, Psa 1:1–3, Tit 2:11–12
- 2Jer 29:13, Deu 4:29, Psa 119:10, Jhn 14:23, Psa 25:10, Ezk 36:27, Pro 23:26, Deu 6:17
- 31Jn 5:18, 1Jn 3:9
- 41Jn 5:3, Jhn 14:21, Mat 28:20, Jer 7:23, Deu 28:1–14, Deu 12:32, Jhn 14:15, Php 4:8–9
- 5Psa 51:10, 2Th 3:5, Heb 13:21, Jer 31:33, Rom 7:22–24, Psa 119:36, Psa 119:32, Psa 119:173
- 61Jn 2:28, Job 22:26, Psa 119:80, Jhn 15:14, Psa 119:31, Psa 119:128, 1Jn 3:20–21, Jas 2:10
- 7Psa 119:171, Psa 119:12, Jhn 6:45, Psa 25:4–5, 1Ch 29:13–17, Psa 25:8–10, Psa 9:1, Isa 48:17
- 8Psa 71:9, Psa 51:11, Php 4:13, Psa 38:21–22, Psa 119:176, Psa 71:18, Psa 119:16, Psa 119:106
- 92Ti 2:22, Jas 1:21–25, 2Ti 3:15–17, Jos 1:7, Psa 119:11, Psa 25:7, Tit 2:4–6, Psa 1:1–3
- 10Psa 119:34, 2Ch 15:15, Psa 23:3, Psa 119:2, Isa 35:8, Psa 119:133, Psa 119:118, Psa 78:37
- 11Psa 37:31, Col 3:16, Psa 40:8, Jer 15:16, Psa 1:2, Job 22:22, Pro 2:10–11, Psa 119:97
- 12Psa 119:64, Luk 24:45, 1Jn 2:27, Psa 25:4–5, Psa 86:11, Psa 119:108, Jhn 14:26, Psa 143:10
- 13Psa 71:15–18, Psa 40:9–10, Psa 37:30, Psa 34:11, Psa 118:17, Psa 119:46, Psa 119:172, Act 4:20
- 14Mat 13:44, Jer 15:16, Psa 119:162, Psa 19:9–10, Psa 112:1, Job 23:12, Psa 119:127, Psa 119:111
- 15Psa 1:2, Jas 1:25, Psa 119:148, Psa 119:97, Psa 119:48, Psa 119:78, Psa 119:131, Psa 119:117
- 16Psa 119:24, Psa 119:47, Pro 3:1, Rom 7:22, Psa 119:35, Psa 119:83, Heb 10:16–17, Psa 119:77
- 17Psa 13:6, Tit 2:11–12, Eph 2:4–5, Psa 116:7, Psa 119:65, Psa 119:124, Eph 2:10, 2Co 9:7–11
- 18Eph 1:17–18, Act 26:18, Isa 32:3, Isa 35:5, Mat 13:13, Mat 16:17, 2Co 4:4–6, Jhn 9:39
- 191Ch 29:15, Psa 39:12, Heb 11:13–16, Psa 119:10, Luk 24:45, Isa 63:17, 2Co 5:6, 1Pe 2:11
- 20Psa 42:1–2, Psa 84:2, Job 23:11–12, Psa 63:1, Psa 119:131, Psa 119:40, Psa 119:174, Rev 3:15–16
- 211Pe 5:5, Psa 119:10, Psa 119:118, Luk 18:14, Deu 28:15, Deu 30:19, Luk 14:11, Mal 4:1
- 22Psa 39:8, Psa 119:39, 1Pe 2:20, 1Pe 4:14–16, 1Pe 3:16–17, Job 16:20, Psa 37:6, 2Sa 16:7–8
- 23Psa 2:1–2, Luk 23:10–11, 1Sa 22:7–13, Luk 22:66, 1Sa 20:31
- 242Ti 3:15–17, Psa 119:92, Col 3:16, Psa 119:16, Jos 1:8, Pro 6:20–23, Psa 19:11, Psa 119:97–100
- 25Deu 30:6, Psa 71:20, Psa 119:159, Col 3:2, Psa 143:11, Psa 44:25, Rom 7:22–24, Psa 119:40
- 26Psa 86:11, Psa 25:4, Psa 27:11, Psa 32:5, Psa 25:8–9, Pro 28:13, Psa 119:12, Psa 38:18
- 27Psa 145:5–6, Psa 105:2, Psa 71:17, Rev 15:3, Psa 78:4, Act 2:11, Psa 111:4, Exo 13:14–15
- 28Php 4:13, Psa 27:14, 1Pe 5:10, Psa 22:14, Isa 40:29, Zec 10:12, Psa 107:26, Psa 29:11
- 291Jn 2:4, Pro 30:8, 1Jn 1:8, Psa 119:37, Heb 8:10–11, Eph 4:22–25, Rev 22:15, Jon 2:8
- 30Jhn 3:19–21, Psa 119:29, Pro 1:29, Luk 10:42, Jos 24:15, 1Pe 2:2, 2Jn 1:4, Deu 11:18–20
- 31Rom 5:5, Pro 23:23, Jhn 8:31, Act 11:23, Isa 45:17, Psa 25:2, 1Jn 2:28, Psa 25:20
- 321Ki 4:29, 2Co 3:17, Heb 12:1, Jhn 8:32, Psa 18:36, Jhn 8:36, Isa 61:1, Psa 119:45
- 33Psa 119:26–27, 1Jn 2:27, Isa 54:13, Php 1:6, Psa 119:12, Mat 24:13, Jhn 6:45, 1Co 1:7–8
- 34Mat 7:24, Jas 1:5, Pro 2:5–6, Psa 119:73, Jas 1:25, Jhn 7:17, Jas 2:8–12, Psa 119:10
- 35Ezk 36:26–27, Psa 23:3, Psa 25:4, Pro 4:11, Php 2:13, 1Jn 5:3, Pro 8:20, Psa 119:16
- 36Heb 13:5, Luk 12:15, Mrk 7:21–22, 1Ki 8:58, Psa 51:10, Exo 18:21, Col 3:5, 2Pe 2:3
- 371Jn 2:16, Pro 4:25, Isa 33:15, Num 15:39, Job 31:1, Mat 5:28, Psa 119:40, Pro 23:5
- 38Jer 32:39–41, Psa 147:11, 2Co 1:20, Psa 103:17, 2Sa 7:25–29, Psa 103:11, Psa 103:13, Psa 145:19
- 39Psa 119:22, Tit 2:8, 1Ti 3:7, Psa 57:3, Rom 2:2, Psa 39:8, Rev 19:2, Psa 119:43
- 40Psa 119:20, Jhn 10:10, 2Co 7:1, Psa 119:159, Php 3:13–14, Psa 119:25, Psa 119:37, Psa 119:88
- 41Psa 69:16, Psa 119:58, Psa 119:76–77, Luk 2:28–32, Psa 119:132, Psa 106:4–5
- 42Act 27:25, Pro 27:11, Mat 27:63, Psa 119:49, Psa 56:10–11, 2Sa 16:7–8, Psa 119:81, Psa 119:74
- 43Psa 9:4, 1Pe 2:23, Eph 1:13, Psa 119:13, Psa 119:175, Psa 71:17–18, Psa 119:52, Psa 50:16
- 44Psa 119:33–34, Rev 22:11, Rev 7:15
- 45Psa 119:133, Psa 119:94, Pro 4:12, Jas 1:25, Jhn 8:30–36, Jhn 5:39, 2Pe 2:19, Eph 5:17
- 46Rom 1:16, Mat 10:18–19, Act 26:1–2, Mrk 8:38, Dan 3:16–18, 2Ti 1:8, Php 1:20, Psa 138:1
- 47Psa 119:48, Psa 119:97, Psa 119:127, Psa 19:7–10, Psa 119:16, Jhn 4:34, Psa 119:174, Psa 119:167
- 48Psa 119:15, Psa 1:2, Mat 7:21, Jhn 15:14, Jhn 13:17, Ezk 44:12, Jas 1:22–25
- 492Sa 7:25, Psa 106:45, Psa 106:4, Psa 119:81, Psa 105:42, Psa 119:74, 1Pe 1:13, Psa 71:14
- 50Rom 15:4, Jhn 6:63, Psa 94:19, Psa 28:7, Psa 42:11, Heb 6:17–19, Jer 15:16, Psa 27:13
- 51Job 23:11, Jer 20:7, Psa 44:18, Psa 119:157, Psa 119:21, Luk 23:35, Luk 16:14–15, Psa 119:69
- 52Psa 103:18, Psa 77:11–12, Psa 105:5, Deu 1:35–36, Deu 4:3–4, 2Pe 2:4–9, Psa 77:5, Exo 14:29–30
- 53Ezr 9:3, Psa 119:158, Ezr 10:6, Jer 13:17, Php 3:18, Luk 19:41–42, Hab 3:16, Rom 9:1–3
- 54Heb 11:13–16, Gen 47:9, Psa 89:1, Psa 10:1
- 55Psa 63:6, Psa 42:8, Isa 26:9, Job 35:9–10, Psa 139:18, Act 16:25, Gen 32:24–28, Jhn 14:21
- 56Psa 119:165, 1Jn 3:19–24, Psa 18:18–22
- 57Lam 3:24, Psa 16:5, Psa 142:5, Jer 10:16, Psa 73:26, Psa 119:115, Jos 24:18, Jos 24:15
- 58Psa 119:41, Heb 10:22, Psa 119:170, Psa 119:10, Psa 4:6, 1Ki 13:6, Psa 27:8, Psa 119:65
- 592Co 13:5, Ezk 18:28, Lam 3:40, 2Co 12:21, Luk 15:17–20, Hag 1:7, Ezk 18:30, Hag 1:5
- 60Psa 95:7–8, Ecc 9:10, Gal 1:16, Pro 27:1, Ezk 10:6–8
- 61Rom 12:17–21, Psa 119:176, Hos 6:9, Pro 24:29, Psa 119:95, Psa 3:1, 1Sa 26:9–11, Psa 140:5
- 62Act 16:25, Mrk 1:35, Psa 42:8, Psa 119:164, Psa 119:7, Psa 119:147, Rom 7:12, Psa 119:137
- 63Psa 101:6, Pro 13:20, Mal 3:16–18, 1Jn 1:3, Psa 119:79, Psa 119:115, Psa 16:3, Psa 142:7
- 64Psa 33:5, Psa 119:12, Mat 11:29, Psa 119:26, Isa 48:17–18, Psa 145:9, Psa 104:13, Psa 27:11
- 65Psa 119:17, Psa 30:11, Psa 13:6, Psa 16:5–6, Psa 116:7, Psa 18:35, 1Ch 29:14, Psa 23:5–6
- 66Php 1:9, Pro 2:1–9, Jas 3:13–18, 1Ki 3:9, Psa 119:34, Psa 119:160, Mat 13:11, Psa 119:172
- 67Jer 31:18–19, Psa 119:71, Hos 5:15–6:1, Psa 119:75, Psa 119:176, Heb 12:5–11, Rev 3:10, Hos 2:6–7
- 68Psa 119:12, Psa 106:1, Exo 34:6–7, Psa 86:5, Mat 19:17, Psa 107:1, Exo 33:18–19, Mat 5:45
- 69Job 13:4, Mat 5:11–12, Psa 119:157, Psa 109:2–3, Mat 26:59–68, Psa 119:51, Psa 119:58, Psa 119:34
- 70Psa 17:10, Act 28:27, Psa 73:7, Psa 119:16, Isa 6:10, Psa 40:8, Psa 119:35, Rom 7:22
- 71Heb 12:10–11, Psa 119:67, 1Co 11:32, Psa 94:12–13, Isa 27:9
- 72Pro 8:10–11, Psa 19:10, Psa 119:127, Pro 16:16, Psa 119:162, Mat 13:44–46, Psa 119:14, Pro 8:19
- 73Psa 139:14–16, Job 31:15, Psa 138:8, Psa 111:10, 2Ti 2:7, Psa 119:125, Job 32:8, 1Jn 5:20
- 74Psa 66:16, Psa 34:2–6, Psa 119:79, Psa 119:42, Luk 21:33, Gen 32:11–12, Psa 108:7, Mal 3:16
- 75Rev 3:19, Heb 12:10–11, Rom 3:4–5, Psa 89:30–33, Psa 25:10, Psa 119:128, Deu 32:4, Psa 119:62
- 76Psa 106:4–5, Psa 86:5, 2Co 1:3–5
- 77Lam 3:22–23, Psa 119:174, Psa 1:2, Psa 119:41, Psa 119:24, Psa 119:47, Dan 9:18, Heb 8:10–12
- 781Pe 2:20, Psa 119:51, Psa 25:3, Psa 119:23, Jhn 15:25, 1Sa 24:10–12, Jer 50:32, Psa 119:85–86
- 79Psa 119:74, Psa 142:7, Psa 119:63, Psa 7:7
- 80Deu 26:16, 1Jn 2:28, 2Ch 12:14, Psa 119:6, Jhn 1:47, 2Co 1:12, Pro 4:23, Psa 32:2
- 81Psa 84:2, Psa 119:40, Psa 73:26, Psa 119:114, Rev 3:15–16, Psa 119:77, Sng 5:8, Psa 119:42
- 82Psa 69:3, Psa 119:123, Pro 13:12, Psa 90:13–15, Psa 86:17, Lam 2:11, Deu 28:32, Isa 38:11
- 83Job 30:30, Psa 119:176, Psa 119:61, Psa 119:16, Psa 102:3–4, Psa 22:15
- 84Rev 6:10–11, Psa 90:12, Psa 7:6, Psa 39:4–5, Psa 89:47–48, Job 7:6–8
- 85Pro 16:27, Psa 35:7, Jer 18:20, Psa 119:78, Psa 7:15, Psa 36:11, Jer 18:22, Psa 58:1–2
- 86Psa 35:19, Psa 70:5, Psa 35:7, Psa 119:78, Psa 109:26, Rom 7:12, Psa 119:151, Psa 119:138
- 87Mat 10:28, Psa 119:61, Isa 58:2, 1Sa 26:24, Psa 119:51, 2Sa 17:16, 1Sa 20:3, 1Sa 23:26–27
- 88Psa 25:10, Psa 119:25, Psa 119:40, Psa 119:2, Psa 119:159, Psa 119:146, Psa 78:5, Psa 132:12
- 891Pe 1:25, Mat 5:18, Mat 24:34–35, Psa 119:160, Psa 119:152, Psa 89:2, 2Pe 3:13
- 90Psa 100:5, Psa 93:1, Mic 7:20, Psa 148:6, Psa 36:5, Psa 89:1–2, Deu 7:9, Psa 104:5
- 91Isa 48:13, Psa 148:5–6, Jer 33:25, Mat 8:9, Gen 8:22, Mat 5:45, Jdg 5:20
- 92Rom 15:4, Pro 6:22–23, Psa 119:143, Psa 94:18–19, Psa 119:77, Psa 119:24, Psa 27:13
- 93Psa 119:50, Psa 119:16, Jhn 6:63, 1Pe 1:23
- 94Zep 3:17, Act 27:23–24, Isa 64:8–10, Isa 44:2, Psa 119:27, Psa 86:2, Isa 44:5, Psa 119:173
- 95Psa 119:167, Psa 119:31, Psa 119:69, Psa 119:85–87, Act 25:3, Act 23:21, Psa 10:8–10, Psa 119:61
- 96Ecc 2:11, Mat 24:35, Mat 5:18, Ecc 1:2–3, 1Sa 31:4–5, 1Sa 9:2, Mat 22:37–40, Psa 39:5–6
- 97Psa 1:2, Pro 2:10, Psa 119:159, Psa 119:48, Jos 1:8, Deu 17:19, Psa 119:167, Deu 6:6–9
- 98Pro 2:6, Jas 1:25, Psa 119:104–105, Col 3:16, Deu 4:6, Psa 119:11, Deu 4:8, Psa 119:30
- 99Mat 11:25, Mat 13:11, 2Ti 3:15–17, Psa 119:24, Mat 23:24–36, 2Ch 29:15–36, Jer 8:8–9, Jer 2:8
- 100Psa 111:10, Jas 3:13, Job 12:12, Job 15:9–10, Job 28:28, Jer 8:8–9, 1Ki 12:6–15, Job 32:4
- 1011Pe 3:10–11, Pro 1:15, Isa 55:7, Psa 119:104, Isa 53:6, Psa 119:59–60, 1Pe 2:1–2, Tit 2:11–12
- 1021Jn 2:27, Psa 18:21, Pro 5:7, 1Th 2:13, Jer 32:40, 1Jn 2:19, Eph 4:20–24
- 103Pro 8:11, Psa 19:10, Pro 24:13–14, Psa 63:5, Job 23:12, Pro 3:17, Sng 5:1, Sng 1:2–4
- 104Psa 119:128, Pro 8:13, Pro 14:12, Psa 119:98, Psa 97:10, Psa 119:100, Rom 12:9, Psa 101:3
- 105Pro 6:23, Psa 43:3, Psa 18:28, 2Pe 1:19, Job 29:3, Psa 19:8, Eph 5:13
- 106Neh 10:29, Psa 56:12, 2Ki 23:3, 2Co 8:5, Psa 66:13–14, Ecc 5:4–5, Psa 119:115, Mat 5:33
- 107Psa 143:11, Psa 34:19, Psa 119:25, Psa 22:14–18, Psa 119:88, Psa 6:1
- 108Heb 13:15, Hos 14:2, Psa 119:12, Num 29:39, Psa 119:169, Psa 119:130, Psa 119:26
- 109Jdg 12:3, 1Co 15:31, Job 13:14, Psa 119:83, Rom 8:36, 1Sa 20:3, Psa 119:117, 1Sa 19:5
- 110Psa 141:9, Psa 140:5, Psa 119:95, Psa 119:85, Psa 119:10, Psa 10:8–18, Psa 124:6–7, Jer 18:22
- 111Jer 15:16, Psa 119:92, Psa 119:174, Psa 16:5, 1Pe 1:4, Deu 33:4, Psa 119:127, Psa 119:74
- 112Psa 119:33, Psa 141:4, 1Ki 8:58, Jos 24:23, Psa 119:36, Psa 119:44, Php 2:13, 1Pe 1:13
- 113Jas 1:8, Jer 4:14, Isa 55:7, Psa 119:97, Mrk 7:21, 2Co 10:5, Psa 119:103, Psa 94:11
- 114Psa 91:1–2, Psa 32:7, Isa 32:2, Psa 3:3, Psa 130:5–6, Psa 119:81, Psa 119:74, Psa 84:11
- 1151Co 15:33, Psa 6:8, Mat 7:23, Psa 139:19, Psa 119:106, Psa 26:5, Psa 26:9, Mat 25:41
- 116Rom 5:5, Psa 25:2, 1Pe 2:6, Isa 41:10, Rom 10:11, Psa 37:24, Psa 37:17, Psa 54:4
- 117Psa 119:6, Jud 1:24, Jhn 10:28–29, Psa 71:6, Psa 139:10, Psa 17:5, Rom 14:4, Isa 41:13
- 118Psa 119:10, Psa 119:21, Isa 44:20, Rev 18:23, Psa 119:29, Eph 4:22, Eph 5:6, 2Ti 3:13
- 119Mal 3:2–3, Mat 7:23, 1Sa 15:23, Ezk 22:18–22, Mat 3:12, Psa 119:111, Jer 6:30, Psa 119:126–128
- 120Dan 10:8–11, Hab 3:16, Heb 12:28–29, Heb 12:21, Php 2:12, Isa 66:2, Lev 10:1–3, 2Ch 34:21
- 121Psa 18:20–24, 2Sa 8:15, Psa 37:33, 2Co 1:12, 2Pe 2:9, Act 21:16, Psa 75:2, Act 25:10–11
- 122Heb 7:22, Psa 119:21, Job 17:3, Isa 38:14, Pro 22:26–27, Gen 43:9, Psa 36:11, Phm 1:18–19
- 123Psa 130:6, Psa 69:3, Psa 143:7, Psa 119:81–82, Lam 4:17
- 124Psa 119:12, Dan 9:18, Psa 103:10, Psa 119:76–77, Psa 130:7, Psa 69:13, Psa 119:132, Psa 119:26
- 125Jas 3:13–17, 2Co 3:5–6, Psa 119:34, Psa 116:16, Pro 14:8, Jas 1:5, Psa 119:11, Psa 119:66
- 126Jer 8:8, Hab 1:4, Mal 2:8, Psa 9:19, Rom 3:31, Rom 4:14, Mat 15:6, Isa 42:14
- 127Psa 19:10, Mat 13:45–46, Pro 16:16, Pro 3:13–18, Pro 8:11, Psa 119:72, Eph 3:8
- 128Psa 119:104, Rom 7:22, Psa 19:7–8, Pro 30:5, Psa 119:6, Deu 4:8, Rom 7:16, Job 33:27
- 129Psa 139:6, Psa 25:10, Psa 119:18, Isa 25:1, Psa 119:2, Psa 119:146, Psa 119:31, Isa 9:6
- 130Psa 119:105, Pro 6:23, 2Co 4:6, Act 26:18, Psa 19:7, Luk 1:77–79, 2Pe 1:19, Pro 1:22–23
- 131Psa 42:1, Psa 119:20, 1Pe 2:2, Psa 81:10, Isa 26:8–9, Heb 12:14, Psa 119:162, Psa 119:174
- 132Psa 119:124, Psa 106:4, Psa 25:16, Psa 25:18, 1Sa 1:11, Exo 4:31, 2Sa 16:12, 2Th 1:6–7
- 133Psa 17:5, Psa 19:13, Psa 119:116, Psa 32:8, Rom 6:12–14, 1Sa 2:9, Psa 121:3, Rom 7:23–24
- 134Psa 119:122, Psa 56:1–2, Luk 1:74–75, Ezk 11:17–20, Ezk 36:24–27, Psa 56:13, Act 9:31, Psa 142:6
- 135Num 6:25–26, Psa 4:6, Psa 80:7, Psa 80:3, Luk 24:45, Psa 80:19, Job 34:32, Job 36:22
- 136Jer 9:1, Ezk 9:4, Psa 119:158, Psa 119:53, 1Sa 15:11, Jer 9:18, Jer 14:17, Rom 9:2–3
- 137Ezr 9:15, Jer 12:1, Psa 145:17, Dan 9:7, Psa 99:4, Rev 16:7, Neh 9:33, Deu 32:4
- 138Psa 19:7–9, Psa 119:144, Psa 119:86, Deu 4:45, Deu 4:8
- 139Jhn 2:17, Psa 69:9, Act 13:27, 1Ki 19:10, 1Ki 19:14, Mat 22:29, Mat 21:16, Mat 12:3–5
- 140Psa 19:8, Pro 30:5, Psa 12:6, 2Pe 1:21, Rom 7:12, Rom 7:22, Psa 119:128, Psa 18:30
- 141Psa 22:6, 2Co 8:9, Jas 2:5, Luk 9:58, Luk 6:20, Pro 3:1, Psa 40:17, Pro 16:8
- 142Psa 19:9, Psa 119:151, Jhn 17:17, Isa 51:8, Isa 51:6, Psa 119:144, Eph 4:21, Psa 36:6
- 143Job 23:12, Psa 119:107, Psa 119:77, Psa 119:16, Psa 116:3, Psa 119:47, Psa 18:4–5, Psa 130:1
- 1441Pe 1:23–25, Dan 12:10, Psa 119:169, 2Co 4:6, Jer 4:22, Pro 10:21, Psa 119:73, Isa 27:11
- 145Psa 119:10, Jer 29:13, Psa 102:1, Psa 119:106, Psa 119:44, Psa 119:115, Psa 86:4, Psa 142:1–2
- 146Psa 119:134, Tit 2:14, Mat 1:21, Jdg 10:15–16, Tit 3:4–8
- 147Mrk 1:35, Psa 5:3, Psa 130:5–6, Psa 88:13, Psa 119:74, Psa 42:8, Psa 119:81, Psa 56:4
- 148Psa 63:6, Luk 6:12, Lam 2:19, Psa 63:1, Psa 139:17–18, Psa 119:62
- 149Isa 63:7, Psa 51:1, Psa 119:40, Psa 55:2, Psa 109:21, Psa 5:2–3, Psa 119:156, Psa 69:16
- 150Psa 27:2, Pro 28:9, Psa 22:16, Psa 50:17, 2Sa 17:16, Job 21:14, Psa 22:11–13, 1Sa 23:16
- 151Psa 145:18, Psa 119:142, Psa 139:2, Psa 34:18, Psa 75:1, Psa 46:1, Psa 119:138, Mat 1:23
- 152Luk 21:33, Ecc 3:14, Psa 111:7–8, Psa 119:144, Psa 119:160, Psa 89:34–37
- 153Lam 5:1, Psa 119:176, Psa 9:13, Psa 119:159, Psa 119:16, Pro 3:1, Psa 25:19, Psa 119:141
- 154Psa 35:1, Jer 50:34, 1Sa 24:15, Mic 7:9, Psa 119:25, Psa 119:40, Jer 11:20, 1Jn 2:1
- 155Eph 2:17–18, Job 5:4, Rom 3:11, Luk 16:24, Psa 10:4, Isa 46:12, Pro 1:7, Isa 57:19
- 156Psa 86:15, Psa 86:13, Isa 63:7, Psa 51:1, Psa 86:5, 1Ch 21:13, 2Sa 24:14, Isa 55:7
- 1571Co 15:58, Psa 119:51, Act 20:23–24, Job 17:9, Isa 42:4, Job 23:11, Psa 44:17, Psa 7:1
- 158Psa 139:21, Psa 119:53, Psa 119:136, Ezk 9:4, Mrk 3:5
- 159Psa 119:97, Psa 119:153, Neh 5:19, Neh 13:22, 2Ki 20:3
- 160Pro 30:5, 2Ti 3:16, Psa 119:144, Mat 5:18, Psa 119:142, Psa 119:152, Ecc 3:14, Psa 119:86
- 1611Sa 24:9–15, Psa 119:157, 1Sa 26:18, Isa 66:2, Jhn 15:25, Psa 119:23, Psa 4:4, Jer 36:23–25
- 162Jer 15:16, Psa 119:72, Psa 119:111, 1Sa 30:16, Isa 9:3, Pro 16:19
- 163Psa 119:128, Rom 12:9, Pro 6:16–19, Psa 119:29, Amo 5:15, Rev 22:15, Eph 4:25, Pro 30:8
- 164Psa 119:62, Psa 55:17, Psa 97:8, Psa 48:11, Rev 19:2
- 165Pro 3:1–2, Isa 32:17, Isa 26:3, Jhn 14:27, Php 4:7, Gal 5:22–23, 1Pe 2:6–8, Pro 3:23
- 166Gen 49:18, Psa 119:81, Psa 119:174, Psa 50:23, Psa 130:5–7, Jhn 7:17, 1Jn 2:3–4, Psa 24:3–5
- 167Rom 7:22, Psa 40:8, Heb 10:16, Jhn 14:21–24, Jhn 15:9–10, Psa 119:97, Psa 119:111, Psa 119:159
- 168Pro 5:21, Psa 139:3, Psa 44:20–21, Job 34:21, Jer 23:24, Psa 98:8, Rev 2:23, Heb 4:13
- 169Jas 1:5, Psa 119:144–145, Pro 2:3–5, Psa 18:6, 2Ch 1:10, 1Ch 22:12, 2Ch 30:27, Dan 2:21
- 170Psa 119:41, Psa 28:2, Gen 32:9–12, 2Sa 7:25, Psa 89:20–25, Psa 31:2
- 171Psa 94:12, Psa 71:23–24, Psa 71:17, Psa 51:15, Psa 119:7, Psa 50:23
- 172Rom 7:14, Eph 4:29, Psa 37:30, Rom 7:12, Mat 12:34–35, Psa 119:138, Psa 119:142, Col 4:6
- 173Isa 41:10–14, Jos 24:22, Deu 30:19, Psa 119:35, 1Ki 3:11–12, Psa 119:94, 2Co 12:9, Psa 119:111
- 174Psa 119:166–167, Psa 119:16, Psa 1:2, Psa 119:162, Psa 119:111, Psa 119:47, Php 1:23, Rom 7:22–25
- 175Isa 55:3, Psa 51:14–15, Isa 26:8–9, Psa 118:18–19, Isa 38:19, Psa 30:9, Rom 8:28, 1Co 11:31–32
- 176Luk 19:10, Isa 53:6, Luk 15:4–7, Jhn 10:16, Mat 15:24, 1Pe 2:25, Psa 119:93, Mat 18:12–13
Mada katika sura hii
78
Affections, Afflictions and Adversities, Blessing, Blindness, Bottle, Character, Chastisement, Children, Communion, Company, Constancy, Covetousness, Deceit, Decision, Desire, Diligence, Dross, Eternity, Faith, Falsehood, Fear, Fellowship, Forgetting God, Free-Will Offerings, God, Hatred, Heart, Holiness, Hope, Instruction, Integrity, Joy, Knowledge, Lamp, Law, Light, Malice, Man, Meditation, Night, Obedience, Oppression, Peace, Perfection, Persecution, Pit, Poetry, Praise, Prayer, Pride, Psalms, Purity, Quotations and Allusions, Refining, Repentance, Resignation, Righteous, River, Seekers, Self-Examination, Seven, Sin, Sinlessness, Speaking, Stumbling, Temptation, Testimony, Thankfulness, Theft and Thieves, Truth, Vanity, Watchfulness, Wicked (People), Wisdom, Word of God, Worship, Young Men, Zeal, Religious