Zekaria 7
1 Katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Dario, neno la Mwenyezi Mungu lilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu.
2 Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regem-Meleki pamoja na watu wao, kumsihi Mwenyezi Mungu
3 kwa kuwauliza makuhani wa nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?”
4 Kisha neno la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni likanijia kusema:
5 “Waulize watu wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu?
6 Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa mnasherehekea kwa ajili ya nafsi zenu?
7 Je, haya sio maneno ya Mwenyezi Mungu aliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefela zikiwa zimekaliwa na watu?’ ”
8 Neno la Mwenyezi Mungu likamjia tena Zekaria:
9 “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Fanyeni hukumu za haki, onesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi.
10 Msimdhulumu mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’
11 “Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao.
12 Wakaifanya mioyo yao migumu kama gumegume, na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni aliyatuma kwa Roho wake Mtakatifu kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, alikasirika sana.
13 “ ‘Nilipoita, hawakusikiliza; kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
14 ‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ”
Marejeleo mtambuka
93
- 1Neh 1:1, Ezr 6:14–15, Zec 1:1, Hag 2:10
- 2Zec 8:21, 1Ki 13:6, Jer 26:19, 1Sa 13:12, Isa 60:7, Ezr 6:10, Ezr 8:28–30, Zec 6:10
- 3Zec 8:19, Jas 4:8–10, 1Co 7:5, Mat 9:15, Hos 4:6, Mal 2:7, Isa 22:12–13, Ezk 44:23–24
- 4Isa 10:16
- 5Zec 1:12, Isa 58:4–6, 1Co 10:31, Mat 5:16–18, Zec 7:3, Rom 14:17–18, Isa 1:11–12, Mat 6:2
- 61Co 11:20–21, 1Co 11:26–29, Hos 8:13, Col 3:17, 1Ch 29:22, 1Co 10:31, Deu 12:7, 1Sa 16:7
- 7Isa 1:16–20, Jer 17:26, Jer 7:23, Jer 7:5, Isa 55:6–7, Ezk 18:30–32, Jer 32:44, Jer 22:21
- 9Mic 6:8, Psa 82:2–4, Pro 21:3, Jer 7:5, Luk 11:42, Jer 21:12, Deu 10:18–19, Jas 2:13–17
- 10Jer 5:28, Psa 72:4, Isa 1:23, Deu 27:19, 1Jn 3:15, Jas 5:4, Pro 22:22–23, Isa 1:16–17
- 11Neh 9:29, Jer 8:5, Hos 4:16, Jer 35:15, Zec 1:4, Act 7:57, Ezk 3:7, Neh 9:26
- 122Ch 36:16, Ezk 11:19, Neh 9:29–30, Ezk 36:26, Act 28:27, Psa 50:17, Ezk 2:4, Dan 9:11–12
- 13Pro 1:24–28, Jer 14:12, Isa 1:15, Jer 11:11, Mic 3:4, Psa 81:8–12, Jas 4:3, Pro 28:9
- 14Deu 28:33, Jer 23:19, Deu 28:64, Deu 4:27, Jer 5:15, Deu 28:49, Zec 2:6, Lev 26:33
Mada katika sura hii
28
Adamant, Afflictions and Adversities, Church, Commandments, Fasting, Hypocrisy, Impenitence, Integrity, Kindness, Malice, Minister, Christian, Month, Oppression, Poor, Prophecy, Prophets, Regem-Melech, Rulers, Selfishness, Self-Will, Seventy, Sharezer, Sherezer, Temple, Wicked (People), Widow, Word of God, Zechariah (Zecharias)