Yeremia 15
1 Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia: “Hata kama Musa na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende!
2 Nao wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, na wafe; waliowekewa kufa kwa upanga, kwa upanga; waliowekewa kufa kwa njaa, kwa njaa; na waliowekewa kupelekwa uhamishoni, wapelekwe uhamishoni.’ ”
3 Mwenyezi Mungu asema, “Nitatuma aina nne za waangamizi: upanga ili kuua, mbwa ili kukokota mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili wale na waangamize.
4 Nitawafanya wawe machukizo kwa falme zote za dunia kwa sababu ya kile alichofanya Manase mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda huko Yerusalemu.
5 “Ni nani atakayekuhurumia, ee Yerusalemu? Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako? Ni nani atakayesimama ili kuuliza kuhusu hali yako?
6 Umenikataa mimi,” asema Mwenyezi Mungu. “Unazidi kukengeuka. Hivyo nitanyoosha mkono wangu juu yako na kukuangamiza, siwezi kuendelea kukuonea huruma.
7 Nitawapepeta kwa ungo kwenye malango ya miji ya nchi. Nitaleta msiba na maangamizi juu ya watu wangu, kwa maana hawajabadili njia zao.
8 Nitawafanya wajane wao kuwa wengi kuliko mchanga wa bahari. Wakati wa adhuhuri nitamleta mwangamizi dhidi ya mama wa vijana wao wa kiume; kwa ghafula nitaleta juu yao maumivu makuu na hofu kuu.
9 Mama mwenye watoto saba atazimia na kupumua pumzi yake ya mwisho. Jua lake litatua kukiwa bado mchana, atatahayarika na kufedheheka. Wale wote waliobaki nitawaua kwa upanga mbele ya adui zao,” asema Mwenyezi Mungu.
10 Ole wangu, mama yangu, kwamba ulinizaa, mtu ambaye ulimwengu wote unashindana na kugombana naye! Sikukopa wala sikukopesha, lakini kila mmoja ananilaani.
11 Mwenyezi Mungu akasema, “Hakika nitakuokoa kwa kusudi jema, hakika nitawafanya adui zako wakuombe msaada nyakati za maafa na nyakati za dhiki.
12 “Je, mtu aweza kuvunja chuma, chuma kinachotoka kaskazini, au avunje shaba?
13 “Utajiri wako na hazina zako nitavitoa kuwa nyara, bila gharama, kwa sababu ya dhambi zako zote katika nchi yako yote.
14 Nitakufanya uwe mtumwa wa adui zako katika nchi usiyoijua, kwa kuwa katika hasira yangu moto umewashwa utakaowaka juu yako daima.”
15 Wewe unafahamu, Ee Mwenyezi Mungu, unikumbuke na unitunze mimi. Lipiza kisasi juu ya watesi wangu. Kwa uvumilivu wako usiniondolee mbali; kumbuka jinsi ninavyoshutumiwa.
16 Maneno yako yalipokuja, niliyala; yakawa shangwe yangu na furaha ya moyo wangu, kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
17 Kamwe sikuketi katika kundi la wafanyao sherehe, wala kamwe sikujifurahisha pamoja nao; niliketi peke yangu kwa sababu mkono wako ulikuwa juu yangu, na wewe ulikuwa umenijaza hasira.
18 Kwa nini maumivu yangu hayakomi, na jeraha langu ni la kuhuzunisha, wala haliponyeki? Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu, kama chemchemi iliyokauka?
19 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Ukitubu, nitakurejesha ili uweze kunitumikia; ukinena maneno yenye maana, wala si ya upuzi, utakuwa mnenaji wangu. Watu hawa ndio watakaokugeukia, wala si wewe utakayewageukia wao.
20 Nitakufanya wewe uwe ukuta kwa watu hawa, ngome ya ukuta wa shaba; watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa maana mimi niko pamoja nawe kukuponya na kukuokoa,” asema Mwenyezi Mungu.
21 “Nitakuokoa kutoka mikono ya waovu, na kukukomboa kutoka makucha ya watu wakatili.”
Marejeleo mtambuka
161
- 1Ezk 14:14, Ezk 14:20–21, Jer 14:11, Jer 11:14, Psa 106:23, Jer 7:15–16, Exo 32:11–14, Psa 99:6
- 2Jer 43:11, Zec 11:9, Rev 6:3–8, Ezk 5:2, Rev 13:10, Jer 14:12, Ezk 5:12, Isa 24:18
- 3Deu 28:26, Lev 26:22, Lev 26:16, Ezk 14:21, Rev 6:8, Lev 26:25, Jer 7:33, 1Ki 21:23–24
- 4Jer 24:9, 2Ki 23:26–27, 2Ki 24:3–4, 2Ki 21:11–13, 2Ki 21:16–17, Ezk 23:46, Deu 28:25, Jer 29:18
- 5Isa 51:19, Nam 3:7, Jer 21:7, Psa 69:20, Jer 16:5, Lam 2:15–16, 1Sa 17:22, Lam 1:12–16
- 6Jer 7:24, Zep 1:4, Zec 7:11, Hos 11:7, Isa 1:4, Jer 6:11, Jer 1:16, Jer 6:19
- 7Mat 3:12, Jer 51:2, Isa 9:13, Jer 5:3, Isa 41:16, Psa 1:4, Jer 18:21, Jer 8:4–5
- 8Isa 3:25–4:1, Luk 21:35, Jer 4:16, Jer 5:6, Jer 6:4–5
- 91Sa 2:5, Isa 47:9, Amo 8:9–10, Lam 1:1, Jer 44:27, Ezk 5:12, Jer 15:2–3, Lam 4:10
- 10Luk 6:22, Ezk 3:7–9, Psa 120:5–6, Job 3:1–26, Mat 10:21–23, Act 16:20–22, Jer 15:20, Act 17:6–8
- 11Pro 16:7, Jer 29:11–14, Psa 106:46, Psa 37:3–11, Ecc 8:12, Jer 37:3, Jer 40:2–6, Jer 21:2
- 12Job 40:9, Hab 1:5–10, Jer 28:14, Jer 1:18–19, Isa 45:9, Jer 21:4–5
- 13Jer 17:3, Psa 44:12, Isa 52:3, Jer 20:5, Isa 52:5, Jer 15:8
- 14Deu 32:22, Jer 16:13, Psa 21:9, Jer 17:4, Deu 28:36, Deu 28:64, Jer 52:27, Isa 42:25
- 15Psa 69:7–9, Jer 12:3, Luk 21:17, Jer 20:12, Jer 17:16, Neh 13:22, Psa 119:84, Psa 106:4
- 16Rev 10:9–10, Ezk 3:1–3, Psa 119:101–103, Job 23:12, Psa 19:10, Psa 119:111, Psa 119:97, Psa 119:72
- 17Psa 1:1, Lam 3:28, Ezk 3:24–25, Psa 26:4–5, Jer 6:11, 2Co 6:17, Jer 13:17, Psa 102:7
- 18Jer 30:15, Job 34:6, Mic 1:9, Job 6:15–20, Jer 20:7, Psa 6:3, Psa 13:1–3, Jer 14:19
- 19Zec 3:7, Luk 21:15, Lev 10:10, Ezk 44:23, Ezk 22:26, Jud 1:24, Gal 1:10, Heb 5:14
- 20Jer 1:18–19, Ezk 3:9, Psa 46:7, Psa 124:1–3, Act 18:9–10, Jer 1:8, Isa 8:9–10, 2Ti 4:16–17
- 212Co 1:10, Isa 49:24–25, Jer 50:34, Isa 54:17, Isa 29:20, Psa 37:40, Gen 48:16, Psa 27:2
Mada katika sura hii
30
Afflictions and Adversities, Backsliders, Blessing, Company, Doubting, Fan, Fellowship, God, Impenitence, Intercession, Iron, Israel, Prophecies Concerning, Jeremiah, Joy, Minister, Christian, Murmuring, Persecution, Prayer, Punishment, Repentance, Reprobacy, Samuel, Seven, Steel, Sun, Usury, War, Wells, Wicked (People), Word of God