Mwanzo 49
1 Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni, mnizunguke ili niweze kuwaambia yale yatakayowatokea siku zijazo.
2 “Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo; msikilizeni baba yenu Israeli.
3 “Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu; umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo.
4 Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena, kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako, kwenye kitanda changu na kukinajisi.
5 “Simeoni na Lawi ni ndugu: panga zao ni silaha za jeuri.
6 Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, na kukata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda.
7 Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno, nayo ghadhabu yao ni ya ukatili! Nitawatawanya katika Yakobo, na kuwasambaza katika Israeli.
8 “Yuda, ndugu zako watakusifu; mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako; wana wa baba yako watakusujudia.
9 Ee Yuda, wewe ni mwana simba; unarudi toka mawindoni, mwanangu. Kama simba hunyemelea na kulala chini, kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha?
10 Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, hadi aje yeye ambaye milki ni yake, ambaye utii wa mataifa ni wake.
11 Atamfunga punda wake katika mzabibu, naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi; atafua mavazi yake katika divai, majoho yake katika damu ya mizabibu.
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai, meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
13 “Zabuloni ataishi pwani ya bahari na kuwa bandari za kuegesha meli; mpaka wake utapanuka kuelekea Sidoni.
14 “Isakari ni punda mwenye nguvu ambaye amelala kati ya mizigo yake.
15 Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika na jinsi nchi yake inavyopendeza, atainamisha bega lake kwenye mzigo na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu.
16 “Dani atahukumu watu wake kwa haki kama mmoja wa makabila ya Israeli.
17 Dani atakuwa nyoka kando ya barabara, nyoka mwenye sumu kando ya njia, yule aumaye visigino vya farasi ili yule ampandaye aanguke chali.
18 “Ee Mwenyezi Mungu, nautafuta wokovu wako.
19 “Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji, lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa.
20 “Chakula cha Asheri kitakuwa kinono, naye atatoa chakula kitamu kinachomfaa mfalme.
21 “Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru azaaye watoto wazuri.
22 “Yusufu ni mzabibu uzaao, mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi, ambao matawi yake hutanda ukutani.
23 Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili.
24 Lakini upinde wake ulibaki imara, mikono yake ikatiwa nguvu, na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli,
25 kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za juu mbinguni, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi.
26 Baraka za baba yako ni kubwa kuliko baraka za milima ya kale, nyingi kuliko vilima vya kale. Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yusufu, juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake.
27 “Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye njaa kuu; asubuhi hurarua mawindo yake, jioni hugawa nyara.”
28 Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka iliyomfaa.
29 Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti,
30 pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Ibrahimu alinunua liwe mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba.
31 Huko ndiko Ibrahimu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaka na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea.
32 Shamba hilo na pango lililo ndani yake lilinunuliwa kutoka kwa Wahiti.”
33 Baada ya Yakobo kumaliza kutoa maelekezo hayo kwa wanawe, akarudisha miguu yake kitandani, akapumua pumzi ya mwisho, na akakusanywa kwa watu wake.
Marejeleo mtambuka
221
- 1Num 24:14, Jer 23:20, Deu 4:30, Dan 10:14, Rev 4:1, Isa 2:2, Heb 10:24–25, Isa 39:6
- 2Psa 34:11, Pro 8:32, Pro 6:20, Pro 23:22, Pro 4:1–4, Pro 7:1, Pro 1:8–9, Pro 5:1
- 3Deu 21:17, Psa 78:51, Psa 105:36, Gen 29:32, 1Ch 2:1, Num 1:20, 1Ch 5:3, 1Ch 5:1
- 4Gen 35:22, Deu 27:20, 1Ch 5:1, Deu 33:6, Jas 1:6–8, 1Co 5:1, Deu 5:21, Gen 46:8
- 5Gen 34:25–31, Gen 29:33–34, Gen 46:10–11, Pro 18:9
- 6Gen 34:30, Psa 26:9, Psa 16:9, Luk 12:19, Jer 4:19, 2Co 6:14, Psa 64:2, Psa 57:8
- 71Ch 4:24–31, Jos 19:1–9, 1Ch 6:65, 1Ch 4:39–40, Jos 21:1–45, 2Sa 13:22–28, 2Sa 13:15, Pro 27:3
- 8Gen 27:29, 1Ch 5:2, Heb 7:14, Deu 33:7, Psa 18:40–43, Gen 29:35, Jos 10:24, 2Ch 30:11
- 9Num 24:9, Rev 5:5, Num 23:24, Mic 5:8, Hos 5:14, Ezk 19:5, Hos 5:4, 1Co 15:24
- 10Num 24:17, Luk 1:32–33, Isa 9:6, Psa 60:7, Jer 23:5–6, Isa 33:22, Isa 42:1, Zec 10:11
- 11Isa 63:1–3, Rev 7:14, Jol 3:18, 1Ki 4:25, Mic 4:4, 1Ki 4:20, Rev 19:18, 2Ki 18:32
- 13Deu 33:18–19, Gen 30:20, Jos 19:10–16
- 14Gen 30:18, 1Ch 12:32, Deu 33:18, Jos 19:17–23, Jdg 5:15–16, Jdg 10:1
- 152Sa 7:1, Jos 14:15, Ezk 29:18, Jdg 3:11, Mat 23:4, Psa 81:6
- 16Deu 33:22, Gen 30:6, Jdg 18:1–2, Num 10:25, Jdg 13:24–25, Jdg 13:2, Jdg 18:26–27, Jdg 15:20
- 171Ch 12:35, Jdg 18:22–31, Jdg 14:1–15
- 18Isa 25:9, Psa 119:166, Psa 119:174, Mic 7:7, Psa 130:5, Psa 25:5–6, Psa 40:1, 1Th 1:10
- 19Deu 33:20–21, 1Ch 5:11–22, Gen 30:11, 1Ch 3:18–22, 1Ch 5:26, Gen 46:16, Jdg 10:1–11, Num 32:1–42
- 20Deu 33:24–25, Gen 30:13, Gen 46:17, Jos 19:24–31
- 21Deu 33:23, Gen 30:8, Jdg 5:18, Jos 19:32–39, Psa 18:33–34, Mat 4:15–16, Jdg 4:6, Jdg 4:10
- 22Gen 41:52, Psa 128:3, Psa 1:1–3, Jos 16:1–10, Gen 30:22–24, Jos 17:14–17, Gen 46:27, Psa 128:1
- 23Gen 37:24, Psa 118:13, Gen 37:4, Psa 64:3, Gen 37:28, Jhn 16:33, Act 14:22, Gen 37:18
- 24Psa 132:2, Isa 28:16, Psa 132:5, Psa 80:1, Job 29:20, 2Ti 4:17, Psa 18:30, Gen 45:11
- 25Gen 35:11, Gen 28:13, Php 4:19, Gen 43:23, Deu 8:17, Deu 33:13–17, 1Ti 4:8, Deu 33:1
- 26Deu 33:15–16, Hab 3:6, Num 6:2, Psa 89:36, Gen 37:28, Gen 27:27–29, Isa 54:10, Gen 28:3–4
- 27Jdg 20:25, Jdg 20:21, Gen 35:18, Ezk 22:27, Num 23:24, Gen 46:21, 1Sa 11:4–11, Act 20:29
- 28Est 8:11, Ezk 39:8–10, Rev 7:4, Gen 35:22, Num 23:24, Est 8:9, Est 9:1–10, Act 26:7
- 29Gen 50:13, Gen 47:30, Gen 15:15, 2Sa 19:37, Gen 25:8–17, Gen 35:29, Rom 12:6–21, Heb 12:23
- 30Gen 23:8–9, Gen 23:20, Gen 23:16–18
- 31Gen 25:9, Gen 35:29, Gen 50:13, Gen 23:3, Gen 47:30, Gen 23:16–20, Act 7:16
- 32Gen 23:17–20
- 33Gen 49:29, Gen 25:8, Gen 35:29, Jos 24:27–29, Heb 11:22, Gen 49:1, Ecc 12:7, Isa 57:1–2
Mada katika sura hii
64
Adder, Anger, Archery, Asher, Benedictions, Benjamin, Bilhah, Blessing, Bow, Burial, Cave, Character, Church, Company, Dan, Death, Earth, Ephraim, Ephron, Fat, Fellowship, Firstborn, Food, Gad, Gentiles, God, Hamor, Heth, Hills, Homicide, Incest, Instability, Intercession, Isaac, Israel, Issachar, Jacob, Jesus, the Christ, Judah, Levi, Lion, Machpelah, Manasseh, Naphtali, Parents, Persecution, Prosperity, Rebekah (Rebecca), Reuben, Salutations, Scepter (Sceptre), Seekers, Self-Will, Serpent, Shepherd, Shiloh, Sidon, Simeon, Stones, Waiting, Will, Wine, Wolf, Zebulun