2 Mambo Ya Nyakati 33
1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na tano.
2 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliyafukuza mbele ya Waisraeli.
3 Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia ambapo Hezekia baba yake, alikuwa amepabomoa. Pia akasimamisha madhabahu za Mabaali na nguzo za Maashera. Akayasujudia majeshi yote ya angani na kuyaabudu.
4 Akajenga madhabahu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu ambamo Mwenyezi Mungu alikuwa amesema, “Jina langu litadumu Yerusalemu milele.”
5 Katika nyua zote mbili za Hekalu la Mwenyezi Mungu akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la angani.
6 Akawatoa kafara watoto wake kwa kuwapitishia motoni katika Bonde la Ben-Hinomu; akafanya ulozi, uaguzi, na uchawi, akatafuta ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa Mwenyezi Mungu, akaichochea hasira yake.
7 Akachukua ile sanamu aliyoichonga na kuiweka katika Hekalu la Mungu ambalo Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Sulemani, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu, mji niliouchagua kutoka makabila yote ya Israeli, nitaliweka Jina langu milele.
8 Sitaifanya tena miguu ya Waisraeli iondoke tena katika nchi niliyowapa baba zenu, ikiwa watakuwa waangalifu kufanya kila kitu nilichowaamuru kuhusu sheria zote, maagizo na amri zilizotolewa kwa mkono wa Musa.”
9 Lakini Manase akawaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu katika upotovu, kiasi kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliangamiza mbele ya Waisraeli.
10 Mwenyezi Mungu akasema na Manase pamoja na watu wake, lakini hawakumjali.
11 Hivyo Mwenyezi Mungu akaleta juu yao majemadari wa jeshi la mfalme wa Ashuru, ambao walimchukua Manase kwenda kifungoni, wakaweka ndoana katika pua yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli.
12 Katika dhiki yake akamsihi Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na kujinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake.
13 Naye alipomwomba, Mwenyezi Mungu akaguswa na kule kusihi kwake na akasikiliza dua lake. Kwa hiyo akamrudisha Yerusalemu na kwenye ufalme wake. Ndipo Manase akatambua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu.
14 Baadaye akajenga ukuta wa nje wa Mji wa Daudi, magharibi mwa chemchemi ya Gihoni katika bonde, hadi kufikia ingilio la Lango la Samaki na akakizunguka kilima cha Ofeli; pia akaufanya mrefu zaidi. Akawaweka majemadari katika miji yote ya Yuda iliyokuwa imejengewa ngome.
15 Akaondolea mbali miungu ya kigeni pamoja na sanamu kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu. Pia akaondoa madhabahu zote alizojenga katika kilima kilichojengwa Hekalu, na katika Yerusalemu, akazitupa nje ya mji.
16 Kisha akarudisha madhabahu ya Mwenyezi Mungu na kutolea juu yake dhabihu za sadaka za amani pamoja na sadaka za shukrani, naye akawaamuru Yuda wamtumikie Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli.
17 Hata hivyo watu wakaendelea kutoa dhabihu mahali pa juu pa kuabudia, lakini wakawa wakimtolea Mwenyezi Mungu, Mungu wao, peke yake.
18 Matukio mengine ya utawala wa Manase, maombi yake kwa Mungu wake na maneno aliyoambiwa na waonaji walionena naye kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli.
19 Maombi yake, pamoja na jinsi Mungu alivyoguswa na kusihi kwake, pia dhambi zake zote na kukosa uaminifu kwake, pamoja na sehemu alizojenga mahali pa juu pa kuabudia, na kusimamisha nguzo za Ashera na sanamu kabla ya kujinyenyekeza kwake: haya yote yameandikwa katika kumbukumbu za waonaji.
20 Manase akalala na baba zake, akazikwa katika jumba lake la kifalme. Naye Amoni mwanawe akawa mfalme baada yake.
21 Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na mbili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili.
22 Akatenda maovu machoni mwa Mwenyezi Mungu, kama baba yake Manase alivyofanya. Amoni akaabudu na kutoa dhabihu kwa sanamu zote alizokuwa ametengeneza Manase.
23 Lakini tofauti na Manase baba yake, hakujinyenyekeza mbele za Mwenyezi Mungu, badala yake Amoni alijiongeza hatia zaidi.
24 Watumishi wa Amoni wakampangia njama, nao wakamuua ndani ya jumba lake la kifalme.
25 Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamepanga njama dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake.
Marejeleo mtambuka
172
- 12Ki 21:1–18, 1Ch 3:13, Ecc 10:16, Isa 3:4, 2Ch 32:33, Isa 3:12, Mat 1:10, 2Ch 34:1–2
- 22Ch 28:3, Deu 18:9, Ezk 11:12, Ezr 9:14, 2Ki 21:2, Deu 12:31, Lev 18:24–30, 2Ki 17:15
- 3Deu 16:21, Deu 17:3, 2Ch 31:1, 2Ch 30:14, Ecc 9:18, 2Ki 23:5–6, Zep 1:5, 2Ki 18:4
- 42Ch 7:16, Deu 12:11, 1Ki 8:29, 2Ch 6:6, Jer 7:30, 2Ch 33:15, 1Ki 9:3, 2Ch 32:19
- 52Ch 4:9, Ezk 8:7–18, Jer 32:34–35
- 62Ch 28:3, Lev 18:21, Lev 19:31, Lev 20:6, Lev 19:26, 2Ki 21:6, 1Ch 10:13, Isa 47:9–12
- 72Ch 33:4, 2Ch 7:16, 2Ch 33:15, Psa 78:68, 1Ki 11:13, 1Ki 8:44, 1Ki 8:48, Psa 132:13–14
- 82Sa 7:10, Deu 4:40, Deu 30:15–20, 1Ch 17:9, Isa 1:19–20, Deu 8:1, 2Ch 7:17–22, Luk 1:6
- 9Pro 29:12, 2Ch 33:2, 2Ki 24:3–4, 2Ki 17:8–11, 2Ki 21:9–11, Ezk 16:45–47, 2Ki 23:26, Mic 6:16
- 10Jer 25:4–7, Act 7:51–52, Neh 9:29–30, Zec 1:4, Jer 44:4–5, 2Ch 36:15–16
- 11Deu 28:36, 2Ch 36:6, Neh 9:32, Psa 107:10–14, Isa 5:26–30, Isa 7:18–20, 2Ki 25:6, Isa 10:8
- 12Exo 10:3, 2Ch 32:26, Psa 50:15, Luk 18:14–15, 1Pe 5:5–6, Jas 4:10, Act 9:11, Hos 5:15
- 131Ch 5:20, Ezr 8:23, Jer 29:12–13, Dan 4:25, Mat 6:33, Mat 7:7–8, Jer 24:7, Isa 55:6–9
- 14Neh 3:3, 2Ch 27:3, 1Ki 1:33, Neh 12:39, Zep 1:10, 2Ch 32:5, 2Ch 17:19, Neh 3:26–27
- 152Ch 33:3–7, Mat 3:8, 2Ki 21:7, Ezk 18:20–22, Hos 14:1–3, Isa 2:17–21
- 162Ch 29:18, 2Ch 14:4, 1Ki 18:30, 2Ch 30:12, Gen 18:19, 2Ch 33:9, Luk 22:32, Lev 3:1–17
- 172Ch 32:12, 2Ki 15:4, 2Ch 15:17, 1Ki 22:43
- 182Ch 33:19, 2Ch 33:12–13, 2Ch 20:34, Amo 7:12, Isa 30:10, 2Ch 32:32, 2Ki 17:13, 1Ki 15:31
- 19Act 9:11, 1Jn 1:9, Dan 5:22, Jer 44:10, Rom 5:16, Pro 15:8, 2Ch 36:12, Psa 119:67
- 20Mat 1:10, 2Ch 32:33, 1Ch 3:14, 2Ki 21:18–25
- 21Luk 12:19–20, 2Ch 33:1, 2Ki 21:19–24, Jas 4:13–15
- 222Ki 21:20, Isa 44:13–20, 2Ch 34:3–4, Ezk 20:18, 2Ch 33:1–10, 2Ki 21:1–11
- 232Ch 33:12, 2Ch 33:19, 2Ti 3:13, Jer 8:12, 2Ch 28:22, 2Ch 33:1, Jer 7:26
- 24Psa 55:23, 2Ki 21:23–26, 2Ch 25:27–28, 2Ch 24:25–26, Rom 11:22, 2Sa 4:5–12
- 25Num 35:33, Gen 9:5–6, 2Ch 26:1, 2Ch 34:1, Num 35:31, 2Ch 36:1
Mada katika sura hii
34
Afflictions and Adversities, Altar, Amon, Baal, Babylon, Church, Church and State, Fetters, Fish Gate, Gihon, God, Hezekiah, High Places, Hinnom, Iconoclasm, Idolatry, Impenitence, Influence, Israel, Prophecies Concerning, Jerusalem, Josiah, Judgments, Liberality, Manasseh, Ophel, Prayer, Prophets, Repentance, Revivals, Rulers, Sorcery, Temple, War, Word of God