2 Mambo Ya Nyakati 27
1 Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki.
2 Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa Mwenyezi Mungu. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya.
3 Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Mwenyezi Mungu na kufanya kazi kubwa kwenye ukuta katika kilima cha Ofeli.
4 Akajenga miji katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na ngome na minara mwituni.
5 Yothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta mia moja za fedha, kori elfu kumi za ngano, na kori elfu kumi za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu.
6 Yothamu akaendelea kuwa na nguvu kwa sababu alienenda kwa ukamilifu mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wake.
7 Matukio mengine ya utawala wa Yothamu, pamoja na vita vyake vyote na vitu vingine alivyofanya, vimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.
8 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita.
9 Yothamu akalala na baba zake na akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Ahazi mwanawe akawa mfalme baada yake.
Marejeleo mtambuka
32
- 11Ch 3:12, Hos 1:1, 2Ki 15:32–38, Mic 1:1, Isa 1:1, Mat 1:9
- 22Ki 15:34–35, Act 5:13, 2Ch 26:4, Psa 119:120, 2Ch 26:16–21
- 32Ch 33:14, Neh 3:26–27, 2Ch 23:20, Jer 20:2
- 42Ch 11:5–10, Luk 1:39, 2Ch 26:9–10, Jos 14:12–13, 2Ch 14:7
- 5Jer 49:1–6, 2Ch 20:1, 2Sa 10:1–14, Jdg 11:4–33
- 62Ch 26:5, 2Ch 19:3
- 72Ch 32:32–33, 2Ch 20:34, 2Ki 15:36, 2Ch 26:22–23
- 82Ch 27:1
- 92Ki 15:38