Mwanzo 23
1 Sara aliishi miaka mia moja na ishirini na saba (127).
2 Sara akafa huko Kiriath-Arba (yaani Hebroni) katika nchi ya Kanaani, naye Ibrahimu akalia na kumwomboleza Sara.
3 Ndipo Ibrahimu akainuka kutoka pale penye maiti ya mke wake. Akazungumza na Wahiti, akasema,
4 “Mimi ni mpitaji na mgeni miongoni mwenu. Niuzieni sehemu ya ardhi yenu ili niweze kumzika maiti wangu.”
5 Wahiti wakamjibu Ibrahimu,
6 “Bwana, tusikilize. Wewe ni mtawala mkuu sana miongoni mwetu. Zika maiti wako katika kaburi unalolipenda kati ya makaburi yetu. Hakuna mtu wa kwetu atakayekuzuia kaburi lake ili kuzika maiti wako.”
7 Ibrahimu akainuka, akasujudu mbele ya Wahiti, wenyeji wa nchi hiyo.
8 Akawaambia, “Kama mnaniruhusu kumzika maiti wangu, basi nisikilizeni, mkamsihi Efroni mwana wa Sohari kwa niaba yangu
9 ili aniuzie pango la Makpela, lililo mali yake, nalo liko mwisho wa shamba lake. Mwambieni aniuzie kwa bei kamili atakayosema ili liwe mahali pangu pa kuzikia miongoni mwenu.”
10 Efroni Mhiti alikuwa ameketi miongoni mwa watu wake; akamjibu Ibrahimu mbele ya Wahiti wote waliokuwa katika lango la mji:
11 “La, bwana wangu, nisikilize. Nakupa shamba, na pia nakupa pango lililo ndani yake. Nakupa mbele ya watu wangu, uzike maiti wako.”
12 Ibrahimu akasujudu tena mbele ya wenyeji wa nchi,
13 akamwambia Efroni wale watu wakiwa wanasikia, “Tafadhali nisikilize. Nitakulipa fedha za hilo shamba. Kubali kuzipokea ili niweze kumzika maiti wangu.”
14 Efroni akamjibu Ibrahimu,
15 “Nisikilize, bwana wangu, thamani ya ardhi hiyo ni shekeli mia nne za fedha, lakini hiyo ni nini kati yako na mimi? Mzike maiti wako.”
16 Ibrahimu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: shekeli mia nne za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara.
17 Hivyo shamba la Efroni huko Makpela karibu na Mamre, yaani shamba pamoja na pango lililokuwamo, nayo miti yote iliyokuwa ndani ya mipaka ya shamba hilo, vilikabidhiwa
18 kwa Ibrahimu kuwa mali yake mbele ya Wahiti wote waliokuwa wamekuja kwenye lango la mji.
19 Baada ya hayo Ibrahimu akamzika Sara mkewe kwenye pango ndani ya shamba la Makpela karibu na Mamre (huko Hebroni) katika nchi ya Kanaani.
20 Hivyo Wahiti wakamkabidhi Ibrahimu shamba pamoja na pango lililokuwa humo kuwa mahali pa kuzikia.
Marejeleo mtambuka
109
- 2Gen 23:19, Gen 13:18, 1Ch 6:57, Jdg 1:10, Gen 27:41, Num 13:22, 1Sa 20:31, Deu 34:8
- 3Gen 10:15, Gen 23:7, Gen 27:46, Gen 23:5, 1Sa 26:6, 2Sa 23:39, Gen 49:30, Gen 25:10
- 4Heb 11:9, 1Ch 29:15, Gen 17:8, Psa 119:19, Gen 49:30, Act 7:5, Heb 11:13–16, Lev 25:23
- 6Gen 24:35, Gen 14:14, Exo 32:22, Gen 24:18, Gen 13:2, Gen 31:35, Gen 21:22, Gen 42:10
- 7Heb 12:14, Pro 18:24, Gen 19:1, Rom 12:17–18, Gen 18:2, 1Pe 3:8
- 8Luk 7:3–4, Heb 7:26, Gen 25:9, 1Jn 2:1–2, 1Ki 2:17
- 9Rom 12:17, Rom 13:8
- 10Gen 34:24, Gen 34:20, Gen 23:18, Rut 4:1–4, Mat 9:1, Isa 28:6, Job 29:7, Gen 24:10
- 11Luk 19:24, Isa 32:8, Jer 32:7–12, Rut 4:11, Gen 23:18, Gen 23:6, Num 35:30, Rut 4:9
- 12Gen 18:2, Gen 23:7, Gen 19:1
- 13Rom 13:8, 2Sa 24:24, Act 20:35, Gen 14:22–23, Col 4:5, Heb 13:5, Php 4:5–8
- 15Ezk 45:12, Exo 30:15, Exo 30:13
- 16Jer 32:9, Zec 11:12, 1Th 4:6, Ezr 8:25–30, Mat 7:12, Gen 43:21, Exo 30:13, Gen 23:15
- 17Gen 25:9, Gen 50:13, Gen 23:20, Act 7:16, Gen 49:29–32, Rut 4:7–10, Jer 32:7–14, Psa 112:5
- 18Rut 4:1, Gen 34:20, Jer 32:12
- 19Ecc 12:7, Ecc 6:3, Job 30:23, Gen 25:9–10, Gen 47:30, Ecc 12:5, Gen 50:13, Gen 50:25
- 20Jer 32:10–14, Rut 4:7–10, 2Sa 24:24, Gen 49:31–32, 2Ki 21:18, Gen 50:24–25, Gen 50:13, Gen 50:5