Mika 5
1 Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi, kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu. Watampiga mtawala wa Israeli shavuni kwa fimbo.
2 “Lakini wewe, Bethlehemu Efrata, ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye asili yake ni kutoka zamani, kutoka milele.”
3 Kwa hiyo Israeli utaachwa hadi mwanamke aliye na uchungu atakapozaa mwana, na ndugu zake wengine warudi kujiunga na Waisraeli.
4 Atasimama na kulichunga kundi lake katika nguvu ya Mwenyezi Mungu, katika utukufu wa jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wake. Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.
5 Naye atakuwa amani yao. Ukombozi na uharibifu Mwashuru atakapovamia nchi yetu na kupita katika ngome zetu, tutawainua wachungaji saba dhidi yake, hata viongozi wanane wa watu.
6 Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga, nchi ya Nimrodi kwa upanga. Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru atakapoivamia nchi yetu na kuingia katika mipaka yetu.
7 Mabaki ya Yakobo yatakuwa katikati ya mataifa mengi kama umande kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kama manyunyu juu ya majani, ambayo hayamngoji mtu wala kukawia kwa mwanadamu.
8 Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa, katikati ya mataifa mengi, kama simba miongoni mwa wanyama wa msituni, kama mwana simba miongoni mwa makundi ya kondoo, ambaye anaumiza vibaya na kuwararua kila anapopita katikati yao, wala hakuna awezaye kuokoa.
9 Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako, nao adui zako wote wataangamizwa.
10 “Katika siku ile,” asema Mwenyezi Mungu, “nitaangamiza farasi wenu kati yenu, na kubomoa magari yenu ya vita.
11 Nitaiangamiza miji ya nchi yenu, na kuziangusha chini ngome zenu zote.
12 Nitaangamiza uchawi wenu, na hamtapiga tena ramli.
13 Nitaangamiza sanamu zenu, na mawe yenu ya ibada yatoke kati yenu; hamtasujudia tena kazi ya mikono yenu.
14 Nitang’oa nguzo za Ashera kati yenu, na kubomoa miji yenu.
15 Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu, kwa mataifa ambayo hayajanitii.”
Marejeleo mtambuka
106
- 1Lam 3:30, Isa 33:22, Jhn 19:3, Job 16:10, Mat 26:67, Jhn 18:22, 2Co 11:20, 2Ki 25:1–3
- 2Mat 2:6, Jhn 7:42, Luk 1:31–33, Isa 9:6–7, Psa 90:2, Gen 49:10, Isa 11:1, Col 1:17
- 3Rev 12:1–2, Rom 9:27–28, Mat 1:21, Mic 4:7, Hos 11:8, Isa 10:20–21, Mic 4:9–10, Mic 7:13
- 4Isa 40:10–11, Psa 23:1–2, Mic 7:14, Luk 1:32, Jhn 10:27–30, 1Pe 1:5, Rev 11:15, Isa 52:13
- 5Luk 2:14, Jhn 14:27, Zec 10:3, Zec 9:10, Ecc 11:2, Eph 2:14–17, Col 1:20–21, Isa 9:6–7
- 6Isa 14:25, Luk 1:74, Gen 10:8–11, Isa 14:2, 2Ki 19:32–35, 2Ki 17:3–5, 2Ki 15:29, Zep 2:13
- 7Psa 72:6, Isa 44:3, Mic 5:3, Hos 14:5, Deu 32:2, Psa 110:3, Rom 10:20, Jer 14:22
- 8Zec 10:5, Mic 4:13, Zec 12:3, Hos 5:14, Oba 1:18–19, Zec 9:15, Psa 2:8–12, Isa 41:15–16
- 9Psa 21:8, Isa 26:11, Psa 10:12, Isa 11:14, Isa 14:2–4, Isa 1:25, Isa 37:36, 1Co 15:25
- 10Zec 9:10, Hos 14:3, Psa 20:7–8, Psa 33:16–17, Hos 1:7, Jer 3:23, Isa 2:7
- 11Isa 2:12–17, Hos 10:14, Isa 6:11, Amo 5:9, Ezk 38:11, Zec 4:6
- 12Deu 18:10–12, Rev 22:15, Isa 8:19–20, Isa 2:20, Zec 13:2–4, Isa 2:18, Rev 19:20, Isa 2:6–8
- 13Ezk 6:9, Ezk 36:25, Zec 13:2, Isa 2:8, Hos 2:16–17, Ezk 37:23, Hos 14:8, Hos 14:3
- 14Exo 34:13
- 15Psa 149:7, Mic 5:8, 2Th 1:8, Isa 65:12