Mwanzo 29
1 Kisha Yakobo akaendelea na safari yake, na akafika nchi ya watu wa mashariki.
2 Huko akaona kisima katika shamba, pamoja na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu na kisima hicho, kwa sababu walikuwa wakinyweshwa kutoka kisima hicho. Jiwe lililokuwa juu ya mdomo wa kisima lilikuwa kubwa.
3 Kondoo walipokusanyika hapo, wachungaji walilivingirisha jiwe hilo kutoka mdomo wa kisima. Kisha walilirudisha jiwe mahali pake juu ya mdomo wa kisima.
4 Yakobo aliwauliza wachungaji, “Ndugu zangu, ninyi mmetoka wapi?” Wakamjibu, “Tumetoka Harani.”
5 Akawauliza, “Je, mnamfahamu Labani, mjukuu wa Nahori?” Wakamjibu, “Ndiyo, tunamfahamu.”
6 Kisha Yakobo akawauliza, “Je, yeye ni mzima?” Wakasema, “Ndiyo, ni mzima; na hapa yuaja Raheli binti yake akiwa na kondoo.”
7 Akawaambia, “Tazama, jua bado liko juu, si wakati wa kukusanya mifugo. Nywesheni kondoo na mwarudishe malishoni.”
8 Wakamjibu, “Haiwezekani, hadi kondoo wote wakusanyike, nalo jiwe livingirishwe kutoka mdomo wa kisima. Ndipo tutawanywesha kondoo.”
9 Alipokuwa akizungumza nao, Raheli akaja na kondoo wa baba yake, kwa maana alikuwa mchunga kondoo.
10 Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mama yake, pamoja na kondoo wa Labani, alienda na kulivingirisha jiwe kutoka mdomo wa kisima na kuwanywesha kondoo wa mjomba wake.
11 Kisha Yakobo akambusu Raheli, na akaanza kulia kwa sauti.
12 Yakobo alikuwa amemwambia Raheli kuwa yeye alikuwa jamaa ya baba yake, na kwamba ni mwana wa Rebeka. Basi Raheli alikimbia na kumweleza baba yake.
13 Mara Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo, mwana wa ndugu yake, aliharakisha kwenda kumlaki. Akamkumbatia na kumbusu, halafu akamleta nyumbani mwake, naye Yakobo akamwambia mambo hayo yote.
14 Ndipo Labani akamwambia, “Wewe ni mwili wangu na damu yangu mwenyewe.” Yakobo awaoa Lea na Raheli Baada ya Yakobo kukaa kwa Labani mwezi mzima,
15 Labani akamwambia, “Kwa vile wewe ni jamaa yangu, ndiyo sababu unifanyie kazi bila ujira? Niambie ujira wako utakuwa nini.”
16 Labani alikuwa na binti wawili; binti mkubwa aliitwa Lea, naye binti mdogo aliitwa Raheli.
17 Lea alikuwa na macho dhaifu, lakini Raheli alikuwa na umbo la kupendeza na mzuri wa sura.
18 Yakobo akampenda Raheli; akamwambia Labani, “Nitakutumikia kwa miaka saba kwa ajili ya kumpata Raheli binti yako mdogo.”
19 Labani akasema, “Ni bora zaidi nikupe Raheli kuliko kumpa mtu mwingine yeyote. Kaa pamoja na mimi hapa.”
20 Kwa hiyo Yakobo akatumika miaka saba ili kumpata Raheli, lakini ilionekana kwake kama siku chache tu kwa sababu ya upendo wake kwa Raheli.
21 Ndipo Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu. Muda wangu umekamilika, nami nataka niingie kwake.”
22 Basi Labani akaalika watu wote wa mahali pale na akafanya karamu.
23 Lakini ilipofika jioni, akamchukua Lea binti yake, akampa Yakobo, naye Yakobo akakutana naye kimwili.
24 Naye Labani akamtoa Zilpa mjakazi wake kuwa mtumishi wa Lea, binti yake.
25 Kesho yake asubuhi, Yakobo akagundua kuwa amepewa Lea! Basi Yakobo akamwambia Labani, “Ni jambo gani hili ulilonitendea? Nilikutumikia kwa ajili ya Raheli, sivyo? Kwa nini umenidanganya?”
26 Labani akajibu, “Si desturi yetu kumwoza binti mdogo kabla ya kumwoza binti mkubwa.
27 Maliza juma la arusi ya binti huyu, kisha pia nitakupa huyu binti mdogo, kwa kutumika miaka mingine saba.”
28 Naye Yakobo akafanya hivyo. Akamaliza juma na Lea, kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake.
29 Labani akamtoa Bilha mjakazi wake kwa Raheli ili kuwa mtumishi wake.
30 Pia Yakobo akakutana na Raheli kimwili, naye akampenda Raheli kuliko Lea. Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka mingine saba.
31 Mwenyezi Mungu alipoona kwamba Lea hapendwi, akamwezesha kupata watoto, lakini Raheli alikuwa tasa.
32 Lea akapata mimba, akazaa mwana. Akamwita jina Reubeni, kwa maana alisema, “Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameona huzuni yangu. Hakika mume wangu sasa atanipenda.”
33 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita jina Simeoni.
34 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Sasa mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita jina Lawi.
35 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Wakati huu nitamsifu Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo akamwita jina Yuda. Kisha akaacha kuzaa watoto.
Marejeleo mtambuka
194
- 1Jdg 6:3, Jdg 6:33, Hos 12:12, Num 23:7, Psa 119:32, Psa 119:60, Ecc 9:7, 1Ki 4:30
- 2Jhn 4:14, Isa 49:10, Jhn 4:6, Gen 24:11, Sng 1:6–7, Rev 7:17, Gen 24:13, Psa 23:2
- 4Gen 28:10, Gen 27:43, Gen 11:31, Act 7:2, Act 7:4, Gen 24:10
- 5Gen 24:24, Gen 24:29, Gen 31:53
- 6Gen 37:14, Exo 18:7, Gen 43:27, 1Sa 25:5, 2Sa 20:9, 1Sa 17:22
- 7Eph 5:16, Gal 6:9–10
- 8Luk 24:2, Mrk 16:3, Gen 29:3, Gen 34:14, Gen 43:32
- 9Exo 2:15–16, Exo 2:21, Sng 1:7–8, Gen 24:15
- 10Exo 2:17
- 11Gen 33:4, Gen 43:30, Gen 45:14–15, Gen 45:2, Rom 16:16, Gen 27:26, Exo 18:7, Gen 29:13
- 12Gen 24:28, Gen 13:8, Gen 14:14–16
- 13Gen 24:29, Luk 7:45, Exo 4:27, 2Sa 19:39, Gen 45:15, Rom 16:16, Exo 18:7, Act 20:37
- 142Sa 19:12–13, Gen 2:23, Jdg 9:2, 2Sa 5:1, Mic 7:5, Gen 29:15, Gen 13:8, Gen 29:12
- 15Gen 30:28, Gen 31:7
- 16Gen 49:31, Rut 4:11, Gen 30:19, Gen 31:4, Gen 29:17, Gen 46:15, Gen 29:25–32, Gen 35:23
- 17Gen 12:11, Gen 30:22, Gen 29:18, Pro 31:30, Gen 39:6, Gen 35:24, Gen 24:16, Gen 35:19–20
- 18Hos 12:12, Exo 22:16–17, Gen 34:12, 2Sa 3:14, Gen 29:30, Hos 3:2, Gen 31:41, Gen 29:20
- 19Isa 6:11, Psa 12:2, Isa 6:5
- 201Co 13:7, Hos 12:12, Eph 5:2, Sng 8:6–7, Gen 24:67, 2Co 5:14, Gen 30:26
- 21Jdg 15:1, Gen 4:1, Mat 1:18, Gen 38:16, Gen 29:18, Gen 29:20, Gen 31:41
- 22Rev 19:9, Mat 22:2–10, Rut 4:10–13, Mat 25:1–10, Jdg 14:10–18, Jhn 2:1–10
- 23Mic 7:5, Gen 24:65, Gen 38:14–15
- 24Gen 16:1, Gen 30:9–12, Gen 46:18, Gen 24:59
- 25Mat 7:2, Pro 11:31, Gen 12:18, Rev 3:19, Jdg 1:7, Gen 27:35–36, 1Co 3:13, Jhn 21:17
- 27Lev 18:18, Jdg 14:12, Gen 8:10–12, Jdg 14:10, Mal 2:15, Gen 2:2–3, 1Ti 6:10
- 29Gen 30:3–8, Gen 29:24, Gen 35:22, Gen 37:2, Gen 35:25
- 30Gen 31:41, Gen 29:20, Mat 10:37, Gen 44:27, Gen 31:15, Gen 29:18, Deu 21:15, Gen 29:31
- 311Sa 2:21, Psa 127:3, Deu 21:15, Mat 10:37, 1Sa 1:5, Gen 30:1–2, Gen 20:18–21:2, Gen 29:30
- 32Deu 26:7, Exo 4:31, Exo 3:7, Gen 42:22, Gen 42:27, Luk 1:25, 1Sa 1:11, 1Sa 1:20
- 33Gen 34:25, Gen 30:8, Gen 35:23, Gen 42:24, Gen 30:20, Gen 49:5–6, Gen 30:6, Gen 30:18
- 34Exo 32:26–29, Gen 49:5–7, Num 18:2–4, Gen 34:25, Exo 2:1, Gen 46:11, Deu 33:8–10, Gen 35:23
- 35Gen 49:8–12, 1Ch 5:2, Mat 1:2, Deu 33:7, Gen 35:26, Gen 38:1–30, Gen 43:8–9, Gen 44:18–34
Mada katika sura hii
34
Beauty, Betrothal, Bilhah, Bride, Brother, Childlessness, Children, Contracts, Covetousness, Dishonesty, Family, Father-in-Law, Favoritism, Haran, Hospitality, Incest, Jacob, Laban, Leah, Levi, Lovers, Marriage, Polygamy, Rachel, Reuben, Servant, Seven, Shepherd, Simeon, Thankfulness, Wages, Wife, Women, Zilpah