Kisha wazee pamoja na watu wote waliokuwa langoni wakasema, “Sisi ni mashahidi. Mwenyezi Mungu na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wanawake wawili ambao pamoja waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata na uwe mashuhuri katika Bethlehemu.