Kisha nikaona viti vya utawala vilivyokuwa vimekaliwa na wale waliopewa mamlaka ya kuhukumu. Tena nikaona roho za wale waliokatwa vichwa kwa sababu ya ushuhuda wa Isa na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawakuwa wamemsujudu huyo mnyama wala sanamu yake wala hawakupokea ile chapa yake kwenye paji za nyuso zao au kwenye mikono yao. Wakawa hai na kutawala pamoja na Al-Masihi miaka elfu.