kama Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alivyokuwa amewaamuru Waisraeli. Akaijenga sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati ya Musa: madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna chombo cha chuma kilichotumika. Hapo juu yake wakamtolea Mwenyezi Mungu sadaka za kuteketezwa na kutoa sadaka za amani.