Hivyo Waisraeli wakafanya kama Yoshua alivyowaagiza. Wakachukua mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Mto Yordani, kulingana na idadi ya makabila ya Israeli, kama Mwenyezi Mungu alivyomwambia Yoshua, nao wakayabeba hadi kambini mwao, mahali walipoyatua chini.