“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie: “ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa, wewe ni kama mnyama mkubwa baharini, unapiga maji kwa kishindo katika vijito vyako, unayavuruga maji kwa miguu yako, na kuchafua vijito.