Kamwe msimwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa njia wanayoabudu miungu yao, kwa sababu katika kuabudu miungu yao, wanafanya aina zote za machukizo anayoyachukia Mwenyezi Mungu. Hata huwateketeza watoto wao wa kiume na wa kike motoni kama kafara kwa miungu yao.