Yule afisa alikuwa amemwambia yule mtu wa Mungu, “Tazama, hata kama Mwenyezi Mungu atafungua madirisha ya mbinguni, je, jambo hili litawezekana?” Naye yule mtu wa Mungu alikuwa amemjibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula chochote kati ya hivyo!”