Al-Yasa akasema, “Sikiliza neno la Mwenyezi Mungu. Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Wakati kama huu kesho, kipimo kimoja cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli moja ya fedha, na vibaba viwili vya shayiri kwa shekeli moja ya fedha katika lango la Samaria.”