Yoashi akawaambia makuhani, “Kusanyeni fedha zote zitakazoletwa kama sadaka takatifu kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu, yaani fedha zilizokusanywa watu walipohesabiwa, fedha zilizopokelewa kutokana na nadhiri za watu binafsi, na fedha zilizoletwa kwa hiari hekaluni.