Kisha Sauli akasema, “Nendeni miongoni mwa watu, mwaambie, ‘Kila mmoja wenu aniletee ng’ombe wake na kondoo, mwachinjie hapa na mle. Msitende dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu kwa kula nyama ikiwa na damu ndani yake.’ ” Hivyo kila mmoja akaleta ng’ombe wake jioni ile na kumchinja hapo.