“Hata hivyo, Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa zangu wote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi, na kutoka nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu, na kutoka wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote.