na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa Mwenyezi Mungu siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za Mwenyezi Mungu mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.