MEGA.Bible Tafuta
Kiswahili

The Mission of the Twelve

Biblia Takatifu (Swahili)

Mat 10:5–15

  1. 5 Hawa kumi na wawili, Isa aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria.
  2. 6 Lakini afadhali mshike njia kuwaendea kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea.
  3. 7 Mnapoenda, hubirini ujumbe huu, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’
  4. 8 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure.
  5. 9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba kwenye vifuko vyenu.
  6. 10 Msichukue mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala jozi ya pili ya viatu, wala fimbo, kwa maana mtendakazi anastahili posho yake.
  7. 11 “Mji wowote au kijiji chochote mtakapoingia, tafuteni humo mtu anayestahili, nanyi kaeni kwake hadi mtakapoondoka.
  8. 12 Mkiingia kwenye nyumba, itakieni amani.
  9. 13 Kama nyumba hiyo inastahili, amani yenu na iwe juu yake. La sivyo, amani yenu na iwarudie ninyi.
  10. 14 Kama mtu yeyote hatawakaribisha ninyi, wala kusikiliza maneno yenu, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu mtakapokuwa mnatoka kwenye nyumba hiyo au mji huo.
  11. 15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa miji ya Sodoma na Gomora kustahimili katika hukumu kuliko mji huo.

Mrk 6:7–13

  1. 7 Akawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili, na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu.
  2. 8 Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kwenye mikanda yenu.
  3. 9 Vaeni viatu, lakini msivae nguo ya ziada.
  4. 10 Mkiingia kwenye nyumba yoyote, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.
  5. 11 Kama mahali popote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza, mtakapoondoka huko, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu ili kuwe ushuhuda dhidi yao.”
  6. 12 Kwa hiyo wakaenenda na kuhubiri kwamba inawapasa watu kutubu na kuacha dhambi.
  7. 13 Wakatoa pepo wachafu wengi, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta na kuwaponya.

Luk 9:1–6

  1. 1 Isa kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote,
  2. 2 kisha akawatuma waende wakahubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
  3. 3 Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada.
  4. 4 Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.
  5. 5 Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”
  6. 6 Hivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.