Mataifa walikasirika; nao wakati wa ghadhabu yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa, na kuwapa thawabu watumishi wako manabii, na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”