Kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka.