basi mwe na hakika kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa hayo mbele yenu. Badala yake, watakuwa tanzi na mitego kwenu, mijeledi migongoni mwenu, na miiba machoni mwenu, hata mwangamie kutoka nchi hii nzuri, ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewapa.