Kama wao ni manabii na wanalo neno la Mwenyezi Mungu, basi na wamsihi Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ili vyombo vilivyobaki katika nyumba ya Mwenyezi Mungu na katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na katika Yerusalemu visipelekwe Babeli.