Gideoni akajibu, “Nisamehe, Ee Bwana wangu. Kama Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi yale matendo yake makuu ambayo baba zetu walitusimulia juu yake waliposema, ‘Je, Mwenyezi Mungu hakutupandisha kutoka Misri?’ Lakini sasa Mwenyezi Mungu ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.”