Baraka akakaribia akimfuatia Sisera, Yaeli akatoka kumlaki. Akamwambia, “Njoo, nitakuonesha mtu unayemtafuta.” Hivyo wakaingia ndani ya hema, na tazama, Sisera alikuwa amelala humo akiwa amekufa, na hicho kigingi cha hema kikiwa kimepigiliwa kupitia paji la uso wake.