Tena Waisraeli wakatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. Wakaabudu Mabaali na Maashtorethi, na miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya Waamoni, na miungu ya Wafilisti. Na kwa kuwa Waisraeli walimwacha Mwenyezi Mungu wala hawakuendelea kumtumikia,