Lakini Manase hawakuwafukuza watu wa Beth-Shani na makazi yake, au watu wa Taanaki na makazi yake, au watu wa Dori na makazi yake, au watu wa Ibleamu na makazi yake, au watu wa Megido na makazi yake, kwa kuwa Wakanaani walikuwa wameamua kuishi katika nchi ile.