Kwa hiyo, kama ndimi za moto zinavyoteketeza nyasi, na kama vile majani makavu yanavyozama katika miali ya moto, ndivyo mizizi yao itakavyooza, na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi; kwa kuwa wameikataa Torati ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli.