Mliona kwa macho yenu wenyewe majaribu makubwa, ishara za miujiza na maajabu, mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, ambao kwa huo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, aliwatoa mtoke Misri. Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawafanyia hivyo watu wote ambao mnawaogopa sasa.