Wakamletea Daudi kichwa cha Ish-Boshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, “Hiki hapa kichwa cha Ish-Boshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyejaribu kukuua. Siku hii ya leo Mwenyezi Mungu amemlipizia kisasi mfalme bwana wangu dhidi ya Sauli na uzao wake.”