Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru Mwenyezi Mungu. Nao wakapaza sauti zao, pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu Mwenyezi Mungu, wakisema: “Yeye ni mwema; fadhili zake zadumu milele.” Ndipo Hekalu la Mwenyezi Mungu likajazwa na wingu,