Mfalme akasimama karibu na nguzo yake na kufanya upya agano mbele za Mwenyezi Mungu kwamba atamfuata Mwenyezi Mungu na kuzishika amri zake, maagizo na sheria zake kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, ili kuyatii maneno ya agano yaliyoandikwa katika kitabu hiki.