Katika mwaka wa nane wa utawala wake, alipokuwa angali bado mdogo, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi baba yake. Katika mwaka wake wa kumi na mbili alianza kutakasa mahali pa juu pa kuabudia pa Yuda na Yerusalemu, akiondoa nguzo za Ashera, sanamu za kuchonga, na sanamu za kusubu.