Wakaleta mafahali saba, kondoo dume saba, wana-kondoo dume saba na beberu saba kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya Yuda. Mfalme akawaamuru makuhani, wazao wa Haruni, kuvitoa vitu hivyo sadaka katika madhabahu ya Mwenyezi Mungu.