Naye Hiramu akaongeza kusema: “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na nchi! Amempa Mfalme Daudi mwana mwenye hekima, aliyejaliwa maarifa na busara, ambaye atajenga Hekalu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe.