Kisha Asa akamlilia Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na kusema, “Ee Mwenyezi Mungu, hakuna yeyote aliye kama wewe wa kuwasaidia wasio na nguvu dhidi ya wenye nguvu. Utusaidie, Ee Mwenyezi Mungu, wewe ndiwe Mungu wetu, kwa kuwa tunakutumainia wewe, nasi kwa jina lako tumekuja dhidi ya jeshi hili kubwa. Ee Mwenyezi Mungu, wewe ndiwe Mungu wetu, usiwaache wanadamu wakushinde wewe.”