Kila asubuhi na jioni wao hutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwa Mwenyezi Mungu. Wao huweka mikate juu ya meza takatifu, na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Sisi tunazishika kanuni za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu.