“Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili la Mwenyezi Mungu, naye Mungu wetu akiwa anasikia: Kuweni na bidii kuzifuata amri za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri, na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele.