Jeroboam
Yeroboamu wa Pili, mwana na mrithi wa Yehoashi, na mfalme wa kumi na nne wa Israeli, ambao aliutawala kwa miaka arobaini na mmoja, K.K. 825-784 (2 Fal. 14:23). Alifuata mfano wa Yeroboamu wa kwanza kwa kuidumisha ibada ya ndama za dhahabu (2 Fal. 14:24). Utawala wake ulikuwa wa wakati mmoja na ule wa Amazia (2 Fal. 14:23) na Uzia (15:1), wafalme wa Yuda. Aliwashinda Washami (13:4; 14:26, 27), naye akaieneza Israeli hata mipaka yake ya zamani, kutoka “maingilio ya Hamathi hata bahari ya Araba” (14:25; Amo. 6:14). Utawala wake wa miaka arobaini na mmoja ulikuwa wenye kufanikiwa kuliko wote ambao Israeli ilikuwa imepata kuujua hata wakati huo. Pamoja na fanaka hii yote ya nje, hata hivyo, uovu ulienea sana katika nchi (Amo. 2:6-8; 4:1; 6:6; Hos. 4:12-14). Manabii Hosea (1:1), Yoeli (3:16; Amo. 1:1, 2), Amosi (1:1), na Yona (2 Fal. 14:25) waliishi wakati wa utawala wake. Alikufa, akazikwa pamoja na baba zake (14:29). Alirithiwa na mwanawe Zekaria (tazama).
His name occurs in Scripture only in 2 Kings 13:13; 14:16, 23, 27, 28, 29; 15:1, 8; 1 Chr. 5:17; Hos. 1:1; Amos 1:1; 7:9, 10, 11. In all other passages it is Jeroboam the son of Nebat that is meant.
Maelezo haya yako kwa Kiingereza.
Familia
Ukoo
Matukio
- 824 BCReign of Jeroboam II
- 783 BCDeath of Jeroboam II
Imetajwa katika
1 Mambo Ya Nyakati 5
Hosea 1