Herodias
(Mt. 14:3-11; Mk. 6:17-28; Lk. 3:19), binti wa Aristobulo na Bernike. Alipokuwa akikaa Roma pamoja na mumewe Herode Filipo wa Kwanza na binti yake, Herode Antipa alikutana naye katika mojawapo ya safari zake kwenda mji ule. Alikubali kumwacha mumewe na kuwa mkewe. Baada ya muda, Herode alikutana na Yohana Mbatizaji, aliyetangaza kwa ujasiri kwamba ndoa ile ilikuwa kinyume cha sheria. Kwa ajili ya hayo “akatupwa gerezani,” yamkini katika ngome ya Makaero (tazama), na huko baadaye akakatwa kichwa.
Familia
- Mwenzi
- Herod Antipas, Philip
- Watoto
- Daughter of Herodias
Ukoo
Imetajwa katika
Mathayo 14
Marko 6
Luka 3