The Decree of Cyrus
Biblia Takatifu (Swahili)
2Ch 36:22–23
- 22 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la Mwenyezi Mungu lililosemwa na nabii Yeremia, Mwenyezi Mungu aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi:
- 23 “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi: “ ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. Yeyote kati ya watu wa Mungu miongoni mwenu, Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na awe pamoja naye, wacha apande.’ ”
Ezr 1:1–4
- 1 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la Mwenyezi Mungu lililosemwa na nabii Yeremia, Mwenyezi Mungu aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi:
- 2 “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi: “ ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda.
- 3 Yeyote kati ya watu wa Mungu miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko Yerusalemu.
- 4 Nao wakazi wa popote manusura wanapoishi sasa, wawape manusura fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, na sadaka za hiari kwa ajili ya Hekalu la Mungu huko Yerusalemu.’ ”