MEGA.Bible Tafuta
Kiswahili

The Cursing of the Fig Tree

Biblia Takatifu (Swahili)

Mat 21:18–22

  1. 18 Asubuhi na mapema, Isa alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa.
  2. 19 Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka.
  3. 20 Wanafunzi wake walipoona jambo hili, wakashangaa, wakamuuliza, “Imekuwaje mtini huu kunyauka ghafula?”
  4. 21 Isa akawajibu, “Amin, nawaambia, mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata mkiuambia huu mlima, ‘Ng’oka, ukatupwe baharini,’ litafanyika.
  5. 22 Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea.”

Mrk 11:12–14

  1. 12 Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, Isa alikuwa na njaa.
  2. 13 Akauona mtini kwa mbali, naye akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini.
  3. 14 Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.