MEGA.Bible Tafuta
Kiswahili

Choosing the Twelve Apostles

Biblia Takatifu (Swahili)

Mat 10:1–4

  1. 1 Ndipo Isa akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.
  2. 2 Haya ndiyo majina ya hao mitume kumi na wawili: wa kwanza, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye;
  3. 3 Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo;
  4. 4 Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa.

Mrk 3:13–19

  1. 13 Isa akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia.
  2. 14 Akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa naye, na awatume kwenda kuhubiri
  3. 15 na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu.
  4. 16 Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro);
  5. 17 Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo);
  6. 18 Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,
  7. 19 na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa.

Luk 6:12–16

  1. 12 Ikawa katika siku hizo Isa alienda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.
  2. 13 Kulipopambazuka, akawaita wanafunzi wake, naye akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume:
  3. 14 Simoni (aliyemwita Petro) na Andrea nduguye, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomayo,
  4. 15 Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni aliyeitwa Zelote,
  5. 16 Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda Iskariote, aliyekuwa msaliti.