Zaburi 120
1 Katika dhiki yangu namwita Mwenyezi Mungu, naye hunijibu.
2 Ee Mwenyezi Mungu, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu.
3 Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4 Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.
5 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya mahema ya Kedari!
6 Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7 Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.