Zaburi 87

1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

2 Mwenyezi Mungu anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo.

3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:

4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.”

6 Mwenyezi Mungu ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”

7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”